FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Friday 4 July 2014

TOBA YARABI..... LULU AANIKA UPAJA WAKE MAKUSUDI.... AJIFANYA HAJUI KUMBE ANACHOJICHORESHA TU

GAUNI alilovaa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael hivi karibuni alipokuwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Watu limeonesha kuwatega wanaume hasa wakware kufuatia kuuanika ‘upaja’ wake.


Msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa kaachia 'upaja' wake.
Akiwa ndani ya Ukumbi uliopo ndani ya Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar, Lulu alionekana amevalia gauni refu lakini pembeni likiwa na mpasuo mkubwa ambapo kila alipokaa, mapaja yake yalionekana wazi hivyo kumfanya ahangaike kuyaficha huku wanaume nao wakitumia muda mwingi kumkodolea macho kisha kunong’ona.
“Duh!Haka kabinti kazuri na lile gauni alilovaa ndiyo anawaacha hoi sana wanaume,ile ni kututafuta ubaya na kama ni kututega kafanikiwa kwa silimia 100,” alisikika kijana mmoja akisema.
Paparazi wetu alifanya jitihada za kutaka kuongea na Lulu juu ya mpasuo huo, lakini hakuwa tayari na hata baada ya zoezi la utoaji wa tuzo, aliondoka fasta akiwa na wapambe wake.

No comments:

Adbox