Kumbe ilikuwa ni tabia yake kwenda kwa mdogo wangu huyo wa
kiume ambaye ni mtoto wa shangazi yangu, na kula uroda wakati mimi sipo, nilipata tetesi hizo kutoka kwa housegirl wetu lakini sikuweza kuamini. siku hiyo nilirudi kimya kimya na kujifungia chumba kimoja ambacho kilikuwa hakitumiki, na wote hawakujua kama nilikuwa nipo.
Mara ilipofika ,majira ya saa nne hivi usiku, nilimuona mke wangu ananyata huku akiwa amevaa nguo za ajabu sana, alipita chumba cha house girl na kisha kuzama kwenye chumba cha ndugu yangu huyo wa kiume. nilitoa simu yangu niliyokuwa nayo na kumpiga picha kwa ushahidi zaidi, alipoingia tu na mimi nikaingia alishindwa kuamini na gafla alianza kuomba msamaha, nilimuuliza mke wangu kwani umefanya nini alishindwa kunijibu huku akiendelea kulia na kuomba msamha, nilitoka na kwenda chumbani kwangu kulala, yule mdogo wangu wa kiume alifungasha usiku ule ule na kuondoka na mke wangu hakuweza kulala, iliniuma sana sikuweza kuamini kwani nilimuamini sana mke wangu.Kesho yake sikuweza kuvumilia nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao , kwani ningeweza kumfanya kitu kibaya sana kama ningeendelea kumuona.
Source: New Paradise
No comments:
Post a Comment