FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Wednesday 16 July 2014

MR NICE AFUNGUKA KUHUSU UTAJIRI WAKE WA BILIONI 1.5 NA JINSI ULIVYOTOWEKA GHAFLA

Mr.Nice akifunguka kuhusu utajiri wake ulivyotoweka ghafla!. Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview.

Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu. Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.

“Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema Mr.Nice.

“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana” 

Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.


Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda.

Ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake.

No comments:

Adbox