Siku ya jana kulikuwa na kikao kilichofanyika mkoani Dodoma, kikao kilichowahusishwa wasanii wote wa mkoa wa Dodoma pamoja na watangazaji wa Redio na ma Producer, kikao hicho kilichoitishwa na kamati ya Utoaji tuzo za wasanii wa Dodoma, kikiongozwa na Director wa Movie Mr Suleshi, Boss ngasa pamoja na Emmanuel,
Nia na madhumuni ya kikao hicho ni kuhusu utoaji tuzo ambazo tuzo hizo zimebatizwa kwa jina la kiasili na kuitwa Nyambago Awards ikiwa na maana ya Mashujaa, Ambapo nyambago walikuwaga ni leader wa mtemi mazengo miaka ya nyuma na walifanya mambo makubwa sana na kuwa ni moja ya mashujaa wa kanda ya kati. kikao hicho kilichofanyika takribani masaa 2 ambapo wasanii pamoja na wadau waliojitokeza walifurahishwa na kitendo hicho ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua dhamani ya kazi zao wanazozifanya na kuwapa motisha ya kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuweza kutanua wigo mpana wa kazi zao wazifanyazao. mwisho wa kikao wasanii waliondoka wakiwa wanachekelea kwa kutokea mkombozi anayewadhamini na kuzidi kusisitiza kamati isikate tamaa ili iweze kuwasaidia wasanii hao:
BOSS NGASA & DADDY ZE MNYAMA ...MDAU
AINEA
KATIBU WA NYAMBAGO
PRODUCER DOUBLE Y
ERICK MSHANA MDAU WA ENTERTAINMENT
DIRECTOR SULESHI & BOSS NGASA
PRODUCER KIDDY AKICHANGIA MADA
PRODUCER KID AKIOMBA MWONGOZO
DIRECTOR SULESHI
Matajiri chipukizi mr Emmanuely na Matei Mdogo mmiliki wa Matei Lounge |
No comments:
Post a Comment