FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday 3 July 2014

UTATA WAIBUKA KATI YA AUNT EZEKIEL NA MTANIRI ANAYETABIRI VIFO VYA WASANII




Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel
SIKU chache baada ya Nabii wa Huduma ya Ufufuo, Buza jijini Dar, Yaspi Paul Bendera kutabiri kuwa vifo vya mastaa vitaendelea, staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel amemwaga machozi baada ya kuhusishwa kuwa yeye ndiye anayefuata kufa.

Kupitia gazeti la Ijumaa, Juni 13, mwaka huu, Nabii Bendera alisema ameoneshwa kwamba wasanii 20 wangekufa hivyo kama wanataka kujinusuru, wafike kanisani kwake na kupakwa mafuta. Chanzo kilicho karibu na staa huyo, kilipenyeza habari kuwa, ndugu zake walimpigia simu Aunt ambapo walionesha kuwa na hofu ya kifo ambayo ilimfanya mwigizaji huyo naye aangue kilio mara kwa mara.
Hata hivyo, chanzo kimeeleza kuwa baada nguvu kubwa kutoka kwa marafiki wa karibu wa Aunt akiwemo Wema wamekuwa wakimsihi amuombe Mungu kwani si kwamba picha yake kutumika gazetini ndiyo atakufa wala maneno ya nabii huyo si sababu ya kuamini kwamba kweli vifo hivyo vitatokea.

No comments:

Adbox