FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Saturday, 12 July 2014

Usajili wa Luis Suarez FC Barcelona na rekodi mpya ya gharama za usajili

20140711-165857-61137370.jpg
Baada ya uwepo wa tetesi za kuihama Liverpool kushika hatamu kwa takribani wiki 3 sasa, hatimaye leo hii Luis Suarez amejiunga rasmi na FC Barcelona akitokea Liverpool.
Usajili wa Suarez umeigharimu FC Barcelona kiasi cha £65m kwa mujibu wa mtandao wa Barcelona, na hii ni rekodi kwa Liverpool – Suarez anakuwa mchezaji aliyeuzwa kwa fedha nyingi zaidi na klabu hiyo iliyoshika nafasi ya pili kwenye EPL msimu uliopita.
Suarez ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Ajax, pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji anayeshika nafasi ya nne kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na Neymar.
20140711-173034-63034421.jpg
Hata hivyo pamoja na usajili huo mchezaji huyo hatoweza kuitumikia Barca mpaka adhabu yake ya kufungiwa mechi 8 na kifungo cha miezi 4 kitakapoisha.
Post a Comment
Adbox