FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Monday 14 July 2014

RAY C ASEMA ALIVAMIWA NA KUPIGWA NA CHID BENZ ‘AMECHANGANYIKIWA NA MADAWA’

Msanii wa muziki na mmiliki wa Ray foundation, Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kusema kuwa alhamisi (july 10) alivamiwa na kupigwa na msanii Chid Benz.
Akizungumza na bongo5 leo ,Ray C amesema kuwa Chid Benz anatafutwa na polisi baada ya kufanya tukio hilo.
“kweli alinivamia alhamisi usiku, amenipiga mimi na amefanya uharibifu wa mali, mimi nashangaa usiku navamiwa ata sikujua nani amemuonyesha nyumbani kwangu, mimi nilikuwa namtafuta kwa sababu ya show ya kuelimisha vijana na maswala ya madawa ya kulevya, yeye akalichukulia kivingine kabisa, nahisi amechanganyikiwa na madawa ya kulevya, kweli itakuwa amechanganyikiwa na madawa, hayuko sawa kabisa.
Sasa hivi nina RB yake , kwaiyo anatafutwa na polisi, kokote atakapo kamatwa anawekwa ndani, najua atajifisha lakini ipo siku atakamatwa na polisi tu. Watanzania wanatakiwa kushirikia na polisi ili akamatwe kwa sasabu Chid hayuko sawa kabisa” Alisema Ray C.

No comments:

Adbox