FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Saturday, 19 July 2014

NAFASI YA 10 LEO KWENYE HOT NEWS : NDEGE NYINGINE YATUA KATIKATI YA BARABARA NCHINI UGANDA


Ndege ndogo ikiwa imebeba wafanyakazi wa jeshi la
 Marekani imetua kwa dhalura katikati ya barabara 
nchini Uganda baada ya kuishiwa mafuta.
Philip Mukasa msemaji wa jeshi la polisi nchini

 Uganda amesema ndege hiyo iliyokua imebeba
 abiria
 wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa
ndege hiyo, ilikuwa iliyokua ikielekea Sudani ya 
Kusini baada ya rubani kugundua hakuwa na 
mafuta ya kutosha aliamua kurudi uwanja wa 
kimataifa wa Entebbe ndipo ikabidi itue kwa
 dhalura
 katikati ya barabara kwenye mji wa Mityana uliopo
 kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa 
Kampala.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa, rubani ametua ndege
 kwa dhalura katikati ya barabara na watu wote 
wametoka salama.

Haikujulikana ni kwa nini rubani hakuelekea Sudan
 ya Kusini na badala yake kaamua kutua katikati ya
 barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta.
TUJIKUMBE HABARI ZILIZOFANYA VIZURI SIKU YA JANA
Post a Comment
Adbox