FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Wednesday, 16 July 2014

MAKAVU LIVE: LAZIMA UKAE...HIVI CHID BENZ HUU NI USHAMBA AU JELA INAKUITA?!SHTUKA....


 
Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.

KWAKO,
Rashid Makwilo ‘Chid Benz’. Naamini utakuwa mzima wa afya njema, kama ndivyo unajisikiaje ukiwa mzima wakati kuna wenzako wanalia na afya zao si nzuri kwa sababu yako?

Lengo la kukuandikia barua hii ni kukuweka sawa ingawa nakumbuka mara kadhaa, waandishi mbalimbali wenye nia njema na wewe waliwahi kuandika makala za kukuweka sawa.
Matukio yako ya kupiga watu kila siku si ya kufumbiwa macho kabisa. Tena ingekuwa bora ungekuwa unagombana na wanaume wenzako, lakini wewe unaowaonea watoto wa kike!

Kama una nguvu kwa nini usiombe pambano na Francis Cheka akuonyeshe kazi? Wewe si bondia? Ukorofi huchafua status ya mtu. Inawezekana unajiona mjanja lakini kumbe unafanya mambo ya kijinga.

Hivi juzi tu, ulimshushia kipondo Aisha Kibuye, ambaye inaelezwa ni shabiki wako. Ulimpiga hadi ukasababisha akawa anazimia kila wakati. Sitaki kuzungumzia hilo sana maana ni jambo lililofikishwa mbele ya mahakama.

Lakini nikuulize, raha yako ya kupiga wenzako ni nini? Juzi tena, umemfuata mwanamuziki mwenzako, Ray C nyumbani kwake na kumpiga.
Hao nimewatolea mfano maana ni matukio yaliyoripotiwa, si ajabu huko mtaani una matukio kibao ya kupiga watu. Hivi ni ushamba au jela inakuita?

Kila kukicha unaleta vurugu na wasanii wenzako. Umegombana na wengi kwenye kumbi mbalimbali za starehe. Ni nini unatafuta ndugu? Inatakiwa ujichunguze upya na ubadilike kabla makubwa hayajakukuta!...
Post a Comment
Adbox