FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Saturday 5 July 2014

BAADA YA KUKATA KIPANDE CHA SIKIO LABIBI YAKE, SASA DUDU BAYA AHUSISHWA NA KESI YA UBAKAJI. SOMA HAPA


Marry mtoto wa Kinyakyusa, mwanamke aliyemfukuza kwake
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Marry "Mama wa Kinyakyusa" amedai kuwa eti amekua akiishi kinyumba na msanii wa Bongo Flava Dudubaya kwa muda mrefu lakini hivi karibuni eti alimfukuza nyumbani msanii huyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vyake viovu ikiwemo ubakaji na unyanyasaji, hayo aliyasema kupitia HekaHeka ya Leo Tena (Cloudsfm) 
Mama wa Kinyakyusa anadai alikua anamnyima unyumba Bwana ake wa zamani (DuduBaya) kwa sababu eti Dudu akishalewa pombe anakua mtata matusi kwa wingi na eti DuduBaya anauwezo wa kuishi Bar siku tatu mfululizo huku akitandika kilauri, na akaanza tabia ya kumwingilia kinguvu mara kwa mara dada huyu, alipoona mateso yanazidi akamfukuza Dudu hapo nyumbani kwani hata kodi ya pango eti anailipa yeye Mwanamke, Marry alichukua vitu vyote alivyowahi kumnunulia Dudubaya ikiwemo jeans, fulana na zagazaga nyingine, baada ya tukio hilo Dudu akawa anamfanyia vurugu nyumbani kwake hadi Marry akaamua kwenda polisi kumshtaki.
Hizi ni Nguo za DuduBaya alizonyang'anywa na Maryy.
Jana mchana Dudu akaitwa kituo cha polisi kujielezea lakini sijui aliambiwa nini huko, yote tisa kumi jana usiku wa manane Dudu Baya akiwa ameongozana na washkaji zake huku wakiwa wanaendesha bodaboda kadhaa walifika hadi katika nyumba anayoishi mwanamke maeneo ya Tandale na kufanya vurugu nyingi huku wakijaribu kuvunja mlango bila mafanikio kwani Marry kwa kushirikiana na majirani walipanga mafriji makochi kwenye mlango kwa ndani ili usifunguke na Dudu asiingie ndani, eti baada ya Dudu kufanya sana vurugu ndio wakaamua kuondoka.
DUDUBAYA:
Nilipomuuliza kama kuna ukweli juu ya tuhuma hizi, DuduBaya alikanusha kwa kuruka futi 800 akadai kuwa yeye ndio amemuacha mwanamke na akamwachia nyumba na furniture zote licha yeye kushiriki kwenye manunuzi ya mali hizo.
Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyu kukutwa na Scandal kubwa kubwa, kwani inasemekana anatafutwa na Polisi mwanza kwa tuhuma za kumkata sikio mama yake mkubwa.

No comments:

Adbox