FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Saturday, 5 July 2014

ALI KIBA: BAADA YA KUPOTEA KWENYE GAME ARUDI NA KUMSHUSHIA LAWAMA ALIYEKUA MENEJA WAKE (FRANK GONGA)

Kushoto ni Frank Gonga na Ali Kiba
Ally kiba 4 real baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu hivi karibuni yeye na mdogo wake anayeitwa Abdu Kiba (kwa pamoja wanajiita Kiba square) wali release ngoma inaitwa "Pita mbele" na alipoulizwa sababu za ukimya wake kwenye kipindi cha XXL Ally Kiba alifunguka kuwa moja wapo ni kumpa nafasi mdogo wake ili ashine lakini sababu nyingine ya Ally Kiba kupotea anasema yeye aliingia mkataba wa kusimamiwa kazi zake za muziki na kampuni flani lakini ndani ya Mkataba huo akakabidhiwaa kwa mtu ili asimamie kazi hizo kama meneja, lakini mtu huyo akawa anamuharibia kazi, anagombana na wadau wa Muziki hali hiyo ikasababisha Ali Kiba aamue kukaa pembeni kusubiri mkataba uishe afanye mambo yake.
Kwa wakati huu Mkataba huo umeisha na Ali Kiba yuko huru ndio maana ameungana na Abdu Kiba wakaachia project ya pamoja.
Ali Kiba hajamtaja Meneja huyo lakini inawezekana akawa ni Frank Gonga, naendelea kumtafuta Frank Gonga ili afunguke kuhusu ishu hii.
Post a Comment
Adbox