MTOTO
mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kufunguka kuwa
amekerwa na kitendo cha mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa
(BBA) 2013, Amir Khan Nando kujinadi kuwa aliwahi kuwa ‘mtu’ wake kitu
ambacho si cha kweli.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na Ijumaa kwa juzikati, Lulu alikiri kuwa Nando aliwahi
kumtokea na alimkubalia awe ‘my baby’ wake lakini baada ya kumshtukia
kuwa hana nia nzuri, alimpotezea kabla hawajazama kwenye dimbwi la
mahaba.
“Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kiki kupitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz nilishamgundua nia yake, nimemshangaa kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa mpenzi wake labda alivyonitokea na kumkubalia lakini sikufanya naye chochote kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme hivyo,” alisema Lulu.
Amir Khan Nando akiwa kwenye mahojiano na Global TV Online ndani ya ofisi za Global Publishers
Juzikati, Nando alifanya mahojiano na Global TV Online ambapo awali
alidai ‘kutembea’ na Lulu lakini alipobanwa zaidi aliumauma maneno na
kudai anampenda na yuko tayari kumuoa kwa sababu ana sifa za kuwa mke
(wife material).
Ili kuyapata mahojiano kamili ya Nando, tembelea tovuti ya utaona bango la Global TV, bofya hapo na utapata majibu mengi ambayo staa huyo wa BBA alifunguka pamoja na vipindi vingine vya kusisimua.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

“Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kiki kupitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz nilishamgundua nia yake, nimemshangaa kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa mpenzi wake labda alivyonitokea na kumkubalia lakini sikufanya naye chochote kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme hivyo,” alisema Lulu.
Ili kuyapata mahojiano kamili ya Nando, tembelea tovuti ya utaona bango la Global TV, bofya hapo na utapata majibu mengi ambayo staa huyo wa BBA alifunguka pamoja na vipindi vingine vya kusisimua.
No comments:
Post a Comment