Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es
Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na
majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa
Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina
halikupatikana.
Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
Akizungumzia tukio hilo mbele
ya wanahabari waliokuwa eneo hilo wakisaka habari, Yusuf Ally
ambaye ni mume wa mwanamke aliyefumaniwa alisema:
“Nilikuwa
katika harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama
anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo
jirani yangu.
“Nilipomuuliza
mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba
haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane
humu ndani.
“Ndipo
nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku
ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi.
Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa
eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga.
“Kapteni
Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia mishale ya saa mbili
usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya
mawasiliano na mimi.”
Mgoni akiomba Msamaha.
Yusuf aliendelea kudai kuwa,
ilipotimu saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba Eliza alionekana
akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa hatua za kunyata na kuangalia
kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi akiwa ameshika
kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na machungwa kadhaa.
Alisema muda mfupi baada ya
kuingia, sungusungu mmoja alikwenda kujibanza kwenye dirisha la chumba
na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo alimshuhudia Baba Eliza
akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange, sungusungu huyo akawatonya
wenzake.
Yusuf akazidi kusema kwamba wote
walitoka kichakani na kwenda kuvamia chumbani ambapo walimkuta mkewe
aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa sababu alijua majanga yatatokea
muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya hivyo kiaina.
Baada ya hali kuwa shwari, Kamanda
wa Sungusungu, Kapteni Makumba alianza kumsomea mashitaka jirani huyo
aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na la kusema zaidi ya kuomba radhi
na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye aliyemshawishi na haikuwa amri
yake.
Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya kitanda iliyochafuliwa na mgoni kwa kinyesi.
Sungusungu walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia ya shilingi milioni moja mwenye mke kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.
No comments:
Post a Comment