![]() |
Samahani lakini kwa picha hii |
Baadhi
ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’,
‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’
na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi
wa Mwananchi umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao
ya kijamii yamechochea ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa
za kulevya na zaidi biashara ya ukahaba vyuoni.
Mitandao
ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna
inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi
wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara,
kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara nyingi
huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea ndani.
Mbali
na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi
yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo
vikuu mbalimbali nchini.
Uchunguzi
umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia
mitandao wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja
atakayekubaliana na bei waliyoweka.
Baadhi
ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’,
‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’
na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia
katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo
kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka
pia namba za simu za wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa
utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza
naye kwa kufanya mapatano kabla ya kukubaliana.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
No comments:
Post a Comment