FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Saturday, 8 February 2014

Arsenal, Liverpool hapatoshi ligi kuu


Wachezaji wa Arsenal wakishangilia goli katika mojawapo ya mechi walizocheza ligi kuu ya England
Ligi kuu ya England inaendelea kwa vinara wa ligi hiyo Arsenal kupambana na Liverpool inayoshika nafasi ya nne kati msimamo wa ligi hiyo.
Liverpool inawakaribisha Arsenal katika uwanja wake wa Anfield, ikisaka pointi tatu muhimu ili iweze kujiimarisha zaidi katika kinyang'anyiro cha ligi hiyo, huku Arsenal nayo ikizitaka pointi hizo ili kuzidi kuweka pengo na wapinzani wake wakuu Manchester City na Chelsea zinazowania taji la ubingwa wa ligi hiyo.
Arsenal ina pointi 55, ikifuatiwa na Manchester City na Chelsea zote zikiwa na pointi 53 kila moja, huku Liverpool ikiwa na pointi 47. Timu zote 20 za ligi hiyo zimekwishacheza mechi 24 kabla ya mchezo wa leo.
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia goli katika mojawapo ya mechi zao
Wachezaji Luis Suarez na Daniel Sturridge wanatarajiwa kuisumbua ngome ya Arsenal kutokana na kuimarika kwa kiwango chao cha mchezo na ufungaji magoli dhidi ya timu pinzani.
Olivier Giroud, Santi Carzola, Mesut Ozil na Oxlade-Chamberlain wakihofiwa kulitia msukosuko lango la Liverpool.
Kwa ufupi ni mchezo muhimu kwa kila timu katika kuwania taji la ubingwa wa ligi kuu ya England na pia kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kucheza kombe la mabingwa barani Ulaya.

No comments:

Adbox