BAADA YA KANGA MOKO NDEMBE NDEMBE SASA HIVI NI MWENDO WA T SHIRT NDEMBWE NDEMBWE...!!
KWA muda mrefu, zilisikika sauti za kupiga
vita makundi ya wanawake yaliyosifika kwa kucheza utupu kwa kulowanisha
khanga maji maarufu kama Khanga Moko Ndembendembe lakini sasa imeibuka
nyingine, inayoitwa
Fulana au Tisheti Ndembendembe Uchunguzi wetu wa
miezi kadhaa tangu mwaka jana ulibaini kwamba tayari staili hiyo ya
uchezaji wa muziki wa mwambao kwa kulowanisha tisheti laini nyeupe kwa
maji na kusababisha chuchu kuonekana sawia, inazidi kushika kasi kama
moto wa kifuu Bongo.
Ilibainika kuwa staili hiyo ambayo ilianzia
Pwani ya Kenya, sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini hasa
kwenye ngoma maarufu za ‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika
mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana. Habari zilisema kuwa katika
uchezaji huo, sharti ‘nido’ ya mrembo iwe saa sita ili kuwavutia na
kuwaridhisha wanaume kimahaba ambao kazi yao huwa ni kuwatuza fedha
baada ya kufurahishwa kwa kutazama uchezaji huo na wengine kuondoka nao
kwenda kuvunja amri ya sita.
Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa.
Mamlaka
na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa nguvu zote kwani huo ni mwanzo
mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania na ongezeko la
maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
Credits:habarizaudaku
No comments:
Post a Comment