Headlines za msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Ilala, Rashid Makwilo aka Chid Benz
zinazidi kuchukua nafasi katika mitandao mbalimbali, sasa leo March 20,
2016 mkali Cyril Kamikaze kupitia ukurasa wake wa instagram ameonekana
kuguswa na kuamua kuandika.
‘Mara
nyingi binadamu anapokua kwenye matatizo ndipo kila mtu ana mnyooshea
kidole , kiukweli nina fahamu pressure ya kua mtu maarufu ilivyo na
wakati mwingine kama hauja jipanga vizuri ni kitu kinaweza kukutesa sana
kwa sababu unapo kua mwenyewe na kuwaza inaweza kukupeleka pabaya
kabisa sababu ni presha nzito sana ambayo wengii hawawezi control ata
wewe ambae unaishi maisha ya kawaida ukiingia huku tulipo ungeelewa kwa
sasa najua ni ngumu,kuna wengine wanajatibu kujiua wengine wanarukwa na
akili wakati walikua wazima ila yote ni mambo na matatizo tunayokutana
nayo duniani sometimes the state of mind inakua ngumu kua controlled’ – Cyril
‘Kuna msemo unaosema kabla hujafa hujaumbika ,Ila binadamu tuwe tunajaribu kum push mtu ata kwa uzuri Chid amekuwa akijaribu kutoa nyimbo kadhaa lakini wengi hawakutoa support ya ku post cover yake kama ambavyo hizi picha za afya yake kubadilika zilivyo trend , sio kitu kizuri kuna muda wewe kama binadamu unahitaji kujua kuna kupanda na kushuka kuna magonjwa na afya njema utajiri umaskini hili linamkuta yoyote yule haijalishi kama maarufu ama sio… Wakati huu sio wakumcheka Chid Benz ni muda wakuwa karibu na kum support’ – Cyril
‘Support yako mtanzania hata kumpa moyo kumpokea kwa ku support kazi zake zinaweza mbadilisha chid huyu mnae muona leo na kua a better person ila kejeli na maneno machafu huzidisha mawazo na kumfanya awe vibaya zaidi .. Well najua kaka yangu Rashid uko strong sana,sababu mi napata nafasi ya kuongea nawewe huo mwili wala isiwe sababu ya watu kuona namna gani vipi najua unaweza vuka kwenye hii hali naamini Mungu yuko pamoja na wewe bado nafasi ipo saaana mfalme wa ilala DONT GIVE UP !! #CHIDBENZANAWEZA #HALIYACHIDBENZSIOMWISHOWAKE #SUPPORTCHIDBENZ’ – Cyril
No comments:
Post a Comment