Kama hukupita kwenye post yangu iliyopita Nalimi Mayunga ni Mtanzania aliyeonyesha kipaji chake kwa hali ya juu kwenye shindano la Airtel Trace Music Stars ambalo lilifanyika juzi Nairobi Kenya na kushindanisha nchi kumi na tatu kutoka Afrika.
Anaondoka na Akon kuelekea Marekani kwa
ajili ya kurekodi single yake kama mkataba unavyosema baada ya
kutangazwa mshindi ambapo akiwa kwa Akon, pamoja na kurekodi pia atapata nafasi ya kupewa mafunzo awe mkali zaidi.
Jina lake ndio limepata uzito kwenye
headlines sasa hivi lakini sio kwamba ndio ameanza kuimba leo, kitambo
kidogo amekuwepo bongoflevani na hizi ni baadhi ya nyimbo sauti yake
imesikika.
No comments:
Post a Comment