FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Friday, 28 November 2014

DODOMA BADO YAZIZIMA TUNDU AMEFUNGUKA NA KUSEMA FEDHA HIZI NI ZA NCHI NA MUHONGO AMESEMA UONGO


Lissu: Naomba niseme kuwa Bunge lako limepotoshwa moja kwa moja na Mh. Muhongo Lissu: Kiambatanisho namba 2 sio ushahidi wa standard charted Hong Kong kutambua chochote ila ni hati ya madai. Lissu: Vitambulisho viwili alivyoleta Muhongo ni kesi za mahakama kuu za mwaka huu, hazina ushahidi wowote wa tuhuma zake Lissu: Kwa ushahidi wa taarifa ya kamati na CAG hizi ni pesa za umma, kama zisingekuwa za umma Rais asingeelekeza zilipwe Lissu: Inakuwaje pesa za binafsi zitolewe maamuzi na Rais, Mawaziri, na Magavana? Lissu: PAP waweze kupewa hizi pesa ilibidi wapewe kibali na Waziri Muhongo, lakini haijapata usajili hivyo si kampuni halali. Lissu: Ndani ya siku moja zimetoka bilioni 78, na kama fedha zinazodaiwa ni binafsi kwanini wapewe Viongozi wa Umma na dini? Lissu: Kuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwa hizi ni fedha za umma. TRA, TAKUKURU na CAG wamekiri ni fedha za umma Lissu: Rushwa tupu imetambaa hadi mahakamani, Majaji wanapewa fedha tukiuliza mnasema ahahahha. Lissu: Waziri Mkuu, Tibaijuka , Muhongo na wote waliotajwa walioko humu ndani, tuanze nao maana hawa tunawaweza Lissu:Kuna la kusisitizwa hapa kuhusu BOT,Benki kuu ni huru na haiwezi ikajificha nyuma ya ushauri mbovu wa Mwanasheria mkuu. Lissu: TRA pekee ndio chombo kikuu chenye mamlaka hapa nchini kutoa ushauri juu ya ushuru upi wa kodi ulipwe Lissu: Mwanasheria Mkuu sio mshauri mkuu wa maswala ya kodi hapa nchini ila TRA. Lissu: Kamati inasema Waziri Mkuu awajibike kwakuwa ndiye mwajibikaji mkuu wa shughuli za serikali, hii ni sahihi kabisa. Lissu: Tunamwachaje Waziri wa wizara ya fedha ambaye ndiye mhusika mkuu wa masuala ya fedha? Lissu: Mkuu wa Kitengo cha Financial Intelligence Unit ndani ya Wizara ya Fedha anatakiwa kuwajibika Lissu: Leo yametokea yaliyozungumzwa toka mwaka 1994 kuwa IPTL itakuja kutuumiza Lissu: Tunataka fedha zetu zirudi maana leo haya yanatokea Jakaya Kikwete ndiye Rais wa nchi Lissu: Wakati IPTL inakuja, Rais Kikwete alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, wakati wanasaini mkataba alikuwa Waziri wa Fedha Lissu: Hakuna jambo baya kama Hakimu kupewa milioni 400, na hiyo sio dhihaka ila ni wajibu wetu kuyasema haya.
Post a Comment
Adbox