FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Tuesday, 28 October 2014

UNAAMBIWA YULE BILIONEA WA MADAWA YA KULEVYA ATIKISA DAR, NI MMILIKI WA MABASI,YADAIWA KUNASWA NA UNGA WA MIL 30

Mtikisiko huo umekuja kufuatia maeneo mbalimbali ya jiji kumzungumzia kwa namna mbili, wengine wakifurahia wengine wakisikitika, hasa wanawake wanaoishi maeneo ya Magomeni Kondoa, Dar  ambako mfanyabiashara huyo ndiko kwenye makazi yake.
Sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zilizokamatwa nyumbani kwa Billionea huyo.
AKUTWA NA BUTI
Mbali na sare kwa maana ya mavazi, pia mtuhumiwa huyo alikutwa na viatu vya jeshi hilo maarufu kwa jina la buti nazo zikiwa mpya!

VITU VINGINE
Vitu vingine vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo ni jiko dogo la gesi na gundi ya plastiki, vyote vinaaminiwa kutumika wakati wa kutengeneza kete za unga tayari kwa kusafirisha.
Mharami, mbali na ishu zote hizo, anadaiwa kumiliki maghorofa mawili, Tandale na Magomeni Kondoa jijini Dar, mabasi na magari manne ya kutembelea mwenyewe.

Kamanda  Godfrey Nzowa akizikagua zana zinazotumika kuandaa kete za madawa ya kulevya.
Inadaiwa kuwa, awali askari zaidi ya 20 kutoka Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania walifika kwenye nyumba hiyo kufuatia kutonywa kuwepo kwa unga na kumbana mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake wanne ndani.Ikadaiwa kuwa, mtuhumiwa na wenzake walijaribu kutoroka  walipogongewa mlango na kukataa kufungua.
Moja ya Ghorofa linadaiwa kuwa ni mali ya bilionea, Mharami Mohamed Abadallah ‘Chonji’
WATU WATOKA NA NGUO ZA KULALIA
Ikazidi kudaiwa kuwa, kufuatia milio ya mabomu na risasi, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walitoka kushuhudia wengine wakiwa na nguo za kulalia tu.

Baadhi ya wahalifu wakichukuliwa kutoka Mahakama ya Kisutu.
“Ilikuwa kama saa saba usiku, polisi walinigongea nyumbani kwangu wakasema wanataka kumkamata mhalifu, tukafuatana hadi nyumbani kwa Mharami. Niliwakuta polisi wengine wakiwa na silaha wameizingira nyumba yake, nilichokishuhudia ni ungaunga ukiwa umesambaa chini, wahusika walikamatwa na kufuatana na askari,” alisema mjumbe huyo.
Bilionea Mharami akiwa na wahalifu wenzake wanne chini ya ulinzi mkali ndani ya Mahakama ya Kisutu.
KAMANDA NZOWA SASA
Naye Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa na waandishi wetu ofisini kwake alisema Mharami alishawahi kukamatwa mwaka 2009 kwa kuhusishwa na madawa ya kulevya ambapo alikuwa chini ya uangalizi wa polisi na mahakama.

Watuhumiwa hao wote walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar, wiki iliyopita chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi na askari magereza mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda na walipelekwa mahabusu ya Gereza la Keko, wanatarajiwa kurudi mahakamani Novemba 6, mwaka huu.
Post a Comment
Adbox