FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Friday, 24 October 2014

UNAAMBIWA DIAMOND KUFUNGWA JELA MIAKA MITATU! HABARI KAMILI SOMA HAPA


Ilielezwa kwamba wanaomsaka Diamond na waliowakamata Wasafi ni wanajeshi wa Military Police (MP) ambao waliwabwaga jamaa hao kituoni hapo kisha kuendelea na mambo yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, Camillus Wambura alisema bado hajawasiliana na kituo cha Oysterbay kuhusu suala hilo na hajapata taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya Mkuu wa upelelezi wa Mkoa.

Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
“Uchunguzi unafanywa huko (Oysterbay). Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi katika uchunguzi wa suala hilo.”
Mapema wiki hii, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
Kwa mujibu wa mwanajeshi wa JWTZ ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, taaluma yake ya sheria imemfanya kuchimba kwa undani suala hilo na kugundua kuwa endapo Diamond atapatikana na hatia atapigwa faini au kwenda jela miaka miwili au mitatu au vyote, yaani faini na kifungo.
Post a Comment
Adbox