FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday 2 October 2014

Gari Aina la BMW Alilopewa Kama Zawadi na Maneja Wake Martin Kadinda Lazua Maneno



wema bmw
Achana na lile gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, gari lingine aina ya BMW 545i aliloletewa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kwenye pati ya ‘bethidei’ yake ni utata mtupu na maswali kibao
NYUMBANI KWA MADAM
Pati hiyo ambayo iliandika historia katika ulimwengu maridhawa wa mastaa iliangushwa nyumbani kwa mwanadada huyo, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo alitimiza umri wa miaka 26.
Katika shughuli hiyo, waalikwa ambao sehemu kubwa walikuwa watu wenye majina, walikula na kunywa kuanzia mchana hadi usiku mnene.
NISSAN MURANO
Akiwa Marekani, Diamond alimuagiza mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ apeleke gari aina ya Nissan Morano lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 36 za madafu ikiwa ni zawadi ya jamaa huyo kwa mkewe huyo mtarajiwa.
Alipoliona gari hilo, Wema alipigwa na butwaa huku akimshukuru Diamond ambaye kwa sasa amempachika jina la Chibu baada ya lile la Dangote ‘kueksipaya’.
MANENO KUNTU
Huku akiambatanisha na picha ya gari hilo, kupitia ukurasa wake wa Instagram alimwandikia Wema: “Nilitazama nikupe vingi huenda ingesaidia kukueleza ni kiasi gani napenda nikuone ukiwa umefurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa…lakini tu sina uwezo huo Mumy…tafadhali pokea hicho kidogo hiki nilichojaliwa leo.”
BMW UTATA MTUPU!
Gari aina ya BMW alilokabidhiwa na meneja wake, Martin Kadinda ndilo habari ya mjini huku nyuma yake kukiwa na maswali kibao.
MAMA WEMA AHOJI
Wa kwanza kuhoji alikuwa ni mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ambaye alikataa kwamba Kadinda hawezi kutoa zawadi ya gari kama hilo hivyo minong’ono ikawa ni mingi.
Baada ya kuona hivyo, Kadinda alitoa kadi ya gari hilo lenye namba spesho za usajili ambapo jina la mmiliki lilisomeka Wema Sepetu.
MKONGO ATAJWA
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, maneno yaliendelea kusambaa kama moto wa kifuu kwamba nyuma ya gari kuna stori kubwa inakuja.
Minong’ono mingine ilikwenda mbele zaidi huku jamaa mmoja mfanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Mkongomani) akitajwa kulinunua na kumpa Kadinda akakabidhi.
Baada ya kuona gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 56 za madafu zinaleta utata, kama kawaida yake, Kadinda alikimbilia kwenye ukurasa wake wa Instagram akaandika:
“….Gari hili linatokana na kazi ndogo tuzifanyazo na sapoti kubwa ya watu wanaotutakia mema. Peke yangu nisingeweza bila sapoti yao….”
MSISITIZO
Akizungumza na gazeti hili juu ya sakata hilo, Kadinda alisema kwa msisitizo: “Ni mimi ndiye nimemnunulia Wema hilo gari.”
MASWALI
Huku Kadinda akisisitiza hivyo, waalikwa walibaki na maswali vichwani likiwemo lile linaloulizwa zaidi kwamba iweje yeye (Kadinda) aendeleshe gari la thamani ndogo aina ya Toyota Corola halafu ampe Wema BMW?
“Hapa pana kitu na kitakapobumburuka itakuwa soo, ni bora Kadinda angefunguka ukweli kuliko kuja kunyooshewa vidole baadaye, ngoja tusubiri,” alisikika mmoja wa mastaa walioalikwa (jina kapuni).
GPL

No comments:

Adbox