September 05 zaidi ya watu 35 walipoteza maisha yao kutokana na ajali ya mabus mawili kugongana uso kwa uso eneo la Saba saba ambalo liko nje kidogo na mji wa Musoma,wasanii waliahidi kwenda kutoa misaada kwa watu waliokutwa na matatizo ya ajali hiyo.
Asubuhi ya leo September 08 kabla wasanii kuanza safari ya kurudi Dar walitiza ahadi yao kwa ndugu na jamaa pamoja ma majuruhi wa ajali kwa kuwatembelea katika hospitali ya mkoa wa mara walipolazwa majuruhi hao na kugawana nao kidogo walichokipata kupitia show yao ya Serengeti Fiesta 2014 iliyofanyika jana.
Hii ilikua ni mara ya tatu kwa timu ya Serengeti Fiesta kutoa misaada na fedha kwa Waliojeruhiwa.
No comments:
Post a Comment