FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday 14 August 2014

Mwanaume Mmoja Ameua Watu Sita Baada ya Mkewe Kuchepuka na Wanaume Hao Kingono



www.jogoomtund.blogspot.com 
Mwanaume mmoja ameua watu 6 baada ya mkewe kujihusisha na wanaume hao kingono, kutokana na tukio hilo mwanamume huyo amehukumiwa adhabu ya kifo nchini China. Shao Zongqi, mwenye umri wa miaka 38 alikutwa na hatia baada ya kutekeleza mauaji hayo mwezi January mwaka huu. Kwa muujibu wa mahakama, Shao alipanga kulipiza kisasi baada ya kugundua kua mkewe alikua na mahusiano na wanaume wawili tofauti,shirika la habari la Xinhua limeeleza hayo. Wakati wa sherehe za mwaka mpya wa kichina,Shao alijeruhi wanaume tisa, na kumuua mmoja pamoja na familia yake na wanaume wengine wawili wa jirani,wakati mwanamume mmoja akiwa na mkewe na mtoto wao wa kiume walinusurika katika tukio hilo.
Wakati hukumu hiyo ikitolewa siku ya jumatatu, iliamuriwa Shao alipe kiasi cha yuani 604,000/- sawa na dola za kimarekani 98,000/- kwa familia walio hai ambao waliondokewa na jamaa zao kutokana na shambulio hilo.
Pamoja na kulipa faini hiyo Shao ameapa kukata rufaa kutokana na hukumu hiyo ya kifo inayomkabili. Advertisement

No comments:

Adbox