FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Wednesday 16 July 2014

MAHABA NIUE: SHILOLE KIUNO AMKINGIA KIFUA NUH MZIWANDA,AWAPA DONGO WANAFKI WANAOMTETE NA KUINGILIA MAPENZI YAO



Mwanadada anayefanya vizuri kunako gemu la muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametetea maisha yake ya kimapenzi na Nuh Mziwanda, akisema madai kwamba ni kijana mdogo kuliko yeye, siyo kweli kwani wanalingana umri.


“Mimi na Mziwanda wangu tunalingana kiumri lakini nawashangaa sana wanaonisema kila siku eti ninatembea na Serengeti boy, jamani mpenzi wangu siyo mdogo kwangu, tunalingana umri, ninampenda na yeye ananipenda, hatujali maneno ya watu,”alisema Shilole.

Nuh Mziwanda
Katika kuonyesha mapenzi yake kwa mwanadada huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Mziwanda amejichora tattoo yenye jina la msanii huyo, ambalo haliwezi kufutika

No comments:

Adbox