Stori: Deogratius Mongela
BAADA
ya kuachana na mkewe ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya
Pwani kinachorushwa na Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida,’ mtangazaji wa
kituo cha Televisheni cha TV1, Ezden Jumanne ametaja sifa za mwanamke
atakayekuja kumuoa kama akitaka kufanya hivyo.
Akizungumza
na mwandishi wetu nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar, Ezden alisema
kuwa kutokana na kupitia kipindi kigumu cha kuachana na aliyekuwa mkewe
amedai kuwa hafikirii kuoa kwa sasa lakini kama akija kuoa tena
atamhitaji mwanamke mcha-Mungu, mwenye heshima, asiyemlevi na
atakayejitambua kama ni mke wa mtu.
No comments:
Post a Comment