FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday, 3 July 2014

BAADA YA DOGO JANJA KUWATUSI TIPTOP, WAAMUA KUMSAMEHE. HUU NDO UAMUZI WALIOCHUKUA


Msanii Dogo Janja ambae aliondokaTiptop kwa kishindo na kufanya kazi na Ustaz Juma na Musoma, amerejea tena kambini (Tiptop) baada ya kuona maisha ya mtaani ni magumu
Akielezea kurudi kwake ndani ya Tiptop Madee amesema 
"Mi nilipigiwa simu na babu tale pamoja na Fela kwamba Abduli amekuja, kama miezi miwili imepita, amekuja anasema mkae myamalize, mi nikawaambiwa aah mbona mi sina tatizo, kwasababu mi mbona naongea nae, kwasababu akiwa na tatizo lake ananitumia meseji ananiomba ushauri, sema tu kwa maswala hayo ya kazi sijawahi kuongea nae chochote.
kuna siku alifanya interview namillard alisema. alitubu mambo aliyokuwa anayaongea kwamba ulikuwa ni utoto, na kweli mi nikaangalia kwa haraka haraka umri aliokuwa nao mwanzo na sasa hivi ni vitu viwili tofauti.
jana pia nikakuta hizo taarifa nikawaambia mbona mi sina tatizo, tukamuita maskani jana tukaongea nae fresh, basi mpaka sasa hivi tuko nae, lakini bado hakuna vitu vingi vinavyoendelea, bado mapema sana, tukishakuwa tayari tutawaambia, lakini ukweli ni kwamba Abduli, Dogo Janja amejoin tena kwenye connection yetu , hicho ndio cha msingi, mengine yote tutawapa taarifa"
Dogo Janja pia nae pia alifunguka sababu za kurudi tena kwenye kambi yake aya mwanzo 

"kwasababu kwanza kuna vitu ambavyo namiss katika mziki wangu na pia nimemiss familia yangu ya mwanzo, kuna vitu ambavyo vinamiss katika mziki wangu hata watu wangu wanaona, nakuwa niko tofauti sana na mazingira ya mziki, sawa naweza kuwa na record sana lakini nyimbo naweka ndani tu, lakini tofauti na huku unapangiwa labda utatoa ngoma hii uutatoa ngoma hii hivyo tu"
kuhusu yeye na Ostaz Juma na Musoma
"Mkataba tu uliisha, tuko poa ila mkataba wangu mi na yeye uliisha, tuko fresh" amesema Dogo Janja
Post a Comment
Adbox