FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Sunday, 27 July 2014

ACHENI CHRISTIAN BELLA AZIDI KUTAMBA, HIKI NDICHO MUNGU ALICHOMJAALIA AMBACHO WASANII WA BONGO HAWANA.http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/04/Christian-Bella2.jpgWasalaaam!

Wana jamvi ni ukweli ulio wazi kuwa hapa kwetu music wa dance haupewi muda wa kusikika hewani kama ilivyo bongo flavour!

Na pamoja Music huo kupewa muda wa hewani bado hukaa masikioni mwetu kwa muda fupi baada ya hapo hakuna anaye tamani kuzisikia tena!

Ni tofauti sana na Music wa dance ambao hukosa muda wa hewani lakini umejaa ujumbe na waimbaji wake ni watu wenye vipaji vya hali ya juu tofauti na kule upande wa pili kwa kina Linex ambapo kila mtu anaweza kuimba na huku wakitegemea Kufata juu ya CD.

Christian Bella

Huyu ni Mmoja wa wasanii wa Music wa dance mwenye kipaji cha hali ya juu, pamoja na wasanii wetu wa dance kuimba lakini Christian Bella ni mwisho wa njia na Ni baba yao.

Yeye hupenda kujiita The king of best melody na hakika hili halina pingamizi kwa yeyote anaye fatilia Mziki wa dansi. Ni Msanii ambaye kama ukibahatika kwenye kwenye show zake huwezi kujuta napengine ukaacha kushangilia bongo flavour,maana si wana mziki wote wa dansi wanaweza kuimba kama Christian Bella.

Hakika akiwa anaimba live unaweza ukafikiri yuko studio kumbe ni sauti original. Wana jamvi kama Mtakumbuka Mwaka jana kama sio juzi mwanzoni Christian Bella alicha na bendi ya Akudo Impact na kuondoka kwenda Sweden kama sijakosea na ilisemekana hotorudi.

Nafikiri kuondoka kwake kuli wauma watu wengi wapenda burudani na Music wa Christian Bella nikiwemo Mimi lakini kilicho kuja kunifuta machungu kidogo ni zawadi aliyo kuwa ameicha ambayo ni wimbo wake aliyo mshirikisha Banana Zoro, Asubuhi-Christian Bella ft Banana.

Kwakweli kama mmesikiliza huu wimbo mtakubali jamaa huyu ni King of best Melody maana humo hata Banana alipotezwa na katika huu wimbo napenda sehemu pale Christian Bella anaimba,

"Christian Bella asubuhi imefika,

Jogoo ameshawika kokorikoo...kokooooo...kokorik oooo....

Wafanyakazi wanaenda maofisini.."


Lakini sababu Mungu alipenda tuendelee kupata burudani akamrudisha nchini Christian Bella maana huyu ndio kocha wao. Jamaa aliporudi tuu aka achia kibao kinaitwa Msaliti.

Hakiika humu kaimba hile mbaya na ambaye amepata kusikia hiki kibao atakuwa shahidi. Sasa yuko na Malaika Band hapa ndipo amekuja kwa kasi zaidi kama wana jamvi mmepata kusikia kibao kinaitwa Umeondoka.

Humu kuna sehemu napenda kuisikia sana ana sema,

Umeondokaaaaa,sikujua kama hutorudi.

Wana jamvi leo nime kamilisha kabisa tafiti yangu kuwa ni kweli. Christian Bella ni The King of Best Melody baada ya kusikia Wimbo alio mshirikisha Ommy Dimpozy unaitwa. Nani kama mama, humu wameimba kuhusu umuhimu wa mama na jinsi ambavyo Mama zetu wame hangaika kututunza kwa shida na kuendelea kutupenda.

Kwakweli kwenye wimbo huu wale wenye machozi ya karibu waki usikia wanaweza kumwaga machozi maana Christian Bella humo kapiga melody za hatari sana,Ommy Dimpozi nae kajitahidi sana na kaimba vizuri sana.

Huu ni moja ya nyimbo nzuri sana kama mtapa wasaha wa kuhusikiliza na mtakubaliana nami kuwa Christian Bella is the king of best melody.


Wana jamvi karibu sana kwa mjadala.
Post a Comment
Adbox