FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday, 12 June 2014

Penny 'Mungu ni Mkubwa Ki Ukweli Nilikuwa na Hali Mbaya Kiafya'


MTANGAZAJI wa maarufu wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa ugonjwa uliompiga juzikati ulikuwa ‘serious’ kiasi cha kuona ni Mungu tu amemwokoa. Akichezesha taya na paparazi wetu, Penny alisema anamshukuru Mungu anaendelea vizuri kwani alikuwa na hali mbaya baada ya kubanwa na ugonjwa wa Athma kwa siku tatu nzima akiwa anasaidiwa kupumua na mashine ya oxygen. “Ukweli nilikuwa na hali mbaya huwa nasumbuliwa na Athma mara kwa mara lakini naweza kubanwa kwa siku moja ila ya safari hii imekuja kwa nguvu sana kwa sababu ilikuja na mafua makali jambo lililosababisha nilazwe kwa siku tatu katika Hospitali ya AAR huku nikipumua kwa kutumia mashine, kweli Mungu ni mkubwa, ninaendelea vizuri,”

No comments:

Adbox