
RIYAMA Ali mwigizaji wa kike asiye na kashifa katika tasnia ya filamu
Bongo, amefunguka kwa kusema kuwa kama kuna msanii mwenzake au mtu
mwenye mapenzi naye angependa kama ana sifa kuhusu yeye katika umahiri
wa kuigiza na mengineyo basi atumie nafasi hiyo akiwa hai, haitaji
kusifiwa akifariki kwani anaamini kuwa sifa hizo hatasikia.
“Nasema mapema kabisa sitaki kusifiwa nikifa, sifa mtu uipate ukiwa hai
kama ni faida au kufurahia mwenyewe ujionee lakini nimeshafumba macho
kuna faida gani, sisikii sioni haya ya nini kwangu miye?,”anasema
Riyama.
Msanii huyo amesema kuwa imekuwa tabia kwa baadhi ya wasanii kuleta
maigizo katika misiba ya wasanii inapotokea mara nyingi waonapo
televisheni ujipanga kwa ajili ya kuhojiwa na waandishi basi hata kama
marehemu alikuwa na ugomvi naye basi atajifanya jana kabla ya umauti
walikuwa wote na kumwachia usia kama rafiki.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment