Msanii wa muziki wa bongo flava Msami amemkana kiaina mrembo na msanii
wa bongo movie Irene Uwoya akitia ugumu kukubali moja kwa moja kama ni
wapenzi.
Msami katika mahojiano na Mamu Africa Blog alikuwa mgumu kukubali moja
kwa moja kama wana mahusiano ya mapenzi na Uwoya akisisitiza kuwa mrembo
huyo ni zaidi ya rafiki.
Akaenda mbali zaidi akisema mara kadhaa amekuwa analala na Uwoya kitanda
kimoja hata siku mbili mpaka tatu lakini wanalala mzungu wa nne.
“Unajua Uwoya ni best friend wangu sana
sana,wakati mwingine nakwenda kwake tunapiga stori mpaka
usiku,tunaangusha pamoja hata siku mbili tatu kitanda kimoja lakini huwa
tunalala mzungu wa nne tu” alisema Msami.
Msami aliendelea kuzunguka kuukubali akitumia neno kwa mfano kama ni
wapenzi na Uwoya kukutana kwao ni baada ya kazi zao kwakuwa kila mmoja
ana majukumu yake ya kikazi.
“Unajua kwa mfano tuna imagine kuwa Uwoya ni mpenzi wangu,mara nyingi tunakutana baada ya mihangaiko yetu ya kila siku.
Baada ya danadana za hapa na pale na kubanwa hatimaye Msami akakiri kuwa kweli anatoka kimapenzi na Uwoya.
Aidha Msami amesema anashangaa watu wanaosema kuwa Uwoya anatoka na
Serengeti boy wakati hawaujui ukweli wa jambo hilo,kwakuwa yeye ana umri
mkubwa zaidi ya mrembo huyo.
Amesema amemzidi Uwoya kwa kuzaliwa kwa miezi kadhaa kwahiyo yeye sio Serengeti boy kwakuwa ni mkubwa kwake.
“Nawashangaa watu wanasema eti Uwoya anatoka na Serengeti Boy yaani hata
ukweli hawaujui mimi ni mkubwa nimemzidi miezi kadhaa wanasemaje eti ni
Serengeti Boy waache hizo” Msami alisema.
No comments:
Post a Comment