Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Bongo Flora Mbasha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kikao hicho kiliitishwa na baba wa Mbasha kwa kushirikiana na ndugu wengine wa pande zote mbili.
“Mbasha na mke wake, Flora walikutanishwa sehemu fulani jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kupatanishwa. Kikao kilikuwa kizito, wakubwa wa
familia zote walikuwepo lakini Flora alikataa mara tano kurudi kwenye
ndoa yake.
Juzi Jumapili, Uwazi lilitia timu nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga
jijini Dar na kubahatika kuzungumza na baba na mama wa Mbasha bila
kumpata Mbasha mwenyewe.
Mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maneno alikiri kuwepo kwa kikao
kwa muda wa siku tatu tofauti lakini akasema mambo yalishindikana.
“Mimi nilikuja Dar kutokea Dodoma wiki moja iliyopita baada ya kupata
wito wa mwanangu kuhusu mgogoro wa ndoa. Nilipofika hapa, sikumkuta
Flora, nyumba ilikuwa tupu.
“Kikao kiliitishwa na pande zote mbili, akiwemo Mchungaji Gwajima ambaye
alionekana kusuluhisha mgogoro wao lakini dalili za Flora hazikuonesha
kuwa tayari kurudi kwenye ndoa yake,” alisema mzee huyo.
Emmanuel Mbasha.
KUNA MKONO WA MTU
Mzee Maneno aliendelea kusema: “Mimi kama mtu mzima, nilichokiona katika
ndoa ya mwanangu kuna mkono wa mtu. Ila sasa ametumia mbinu kubwa sana
kumrubuni Flora na yeye kakubali kurubunika.”
MAMA MZAZI NAYE
Kwa upande wake, mama mzazi wa Mbasha, Zulfa Maneno alisema kwake ni
masikitiko makubwa kwa sababu mtoto wake alishakuwa na jina kubwa
kimataifa na mkewe pia.
Alisema: “Mimi kwenye kikao nilipomwona Flora anakataa ndoa yake mara
tano, kila akiulizwa anasema hataki kurudi mpaka mara tano, nikajua
hakuna ndoa.
“Ninachojua, mgogoro huo wa ndoa ulitengenezwa kwa makusudi kabisa ili
ndoa ivunjike. Ila kama aliamua kumwacha mwanangu angefanya hivyo kwa
amani na si visa kama hivi.”
Kuhusu kutakiwa shilingi milioni sitini ili Flora arejee kwenye ndoa
yake, wazazi hao walisema hawajui kitu labda kama yanasemwa pembeni.
Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha.
KULIKUWA NA MGOGORO Habari zaidi zinadai kwamba, fedha zinazotakiwa
kulipwa ni kwa sababu, ndoa hiyo ilikumbwa na mgogoro kabla ya kuibuka
kwa madai ya Mbasha kumbaka shemeji yake.
Flora aliwahi kufungukia hilo kwamba, kabla ya kutokea kwa madai ya
ubakaji, alitibuana na Mbasha na akaamua kuondoka nyumbani kwenda kuishi
hotelini.
DALILI MBAYA
Kuna madai kwamba, siku ambayo Mbasha alikwenda kujisalimisha polisi
(Juni 16, 2014), Flora alipigiwa simu kujulishwa lakini hakutokea
kituoni.
Ikazidi kuelezwa kwamba, siku Mbasha anapelekwa Mahakama ya Wilaya ya
Ilala, Dar kujibu madai ya ubakaji, pia Flora alijulishwa lakini
hakutokea mahakamani hapo.
Mbali na kupelekwa mahakamani, habari za uhakika zinasema hata pale
Mbasha alipokosa dhamana na kupelekwa kwenye Gereza la Keko, Flora
alijulishwa, lakini hakufanya lolote.
“Je, kwa hayo yote ni kweli Flora anaipenda ndoa yake? Si jibu lipo wazi
kwamba hakuna ndoa.” alisema mtu mmoja aliye karibu na familia hiyo.
Mama mzazi wa Emmanuel Mbasha.
MBASHA BAADA YA KUTOKA JELA
Ushahidi wa majirani umeweka bayana kwamba, Mbasha alipotoka gerezani na
kufika nyumbani kwake, Tabata-Kimanga, Dar, walimfuata na kuangua kilio
mbele yake huku wakimpa pole kwa mkasa mzima.
Baadhi ya majirani waliozungumza na Uwazi juzi, walisema kuwa siku hiyo
nyumbani kwa Mbasha kulikuwa na dalili zote za kuwepo kwa msiba kwani
vilio vilitawala.
MADAI
Mbasha, alipandishwa mahakamani Juni 17, mwaka huu kwa madai ya kumbaka mara mbili shemeji yake (jina tunalo).
Siku hiyo alikosa dhamana na kupelekwa Gereza la Keko ambapo Alhamisi ya
Juni 19, mwaka huu alirudishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya
dhamana. Kesi yake itaanza kusikilizwa Julai 17, mwaka huu huku
ikielezwa kuwa upelelezi umekamilika.
Kwa mahojiano kamili ya Mzee Maneno, mkewe na Uwazi fungua Global Tv Online kupitia.CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment