Oohoo nooo! Wakati aliyekuwa mumewe, George Otieno Okumu ‘Tyson’ (41)
akipumzishwa kwenye nyumba ya milele huko Kisumu nchini Kenya,
Yvone-Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ amewacharukia watu waliodai alikuwa
akijipendekeza msibani ili kupata mirathi ya mwanaume huyo.
Awali, Mona ambaye ni staa mkubwa wa sinema za Kibongo alianza kutupia
mitandaoni picha za kumbukumbu (mastaa wanaita Throw Back Thursday au
TBT) akiwa na Tyson kuanzia siku ya send-off yake Agosti 14, 2001 na ile
ya siku ya harusi yao Agosti 25, 2001.
Picha hizo ziliambata na maneno ikionesha ni kwa jinsi gani Tyson au
baba Sonia (mtoto wao) alivyokuwa mtu muhimu maishani mwake.
Ishu hiyo ndiyo iliyosababisha tafrani kubwa huku akiambulia kushambuliwa kwa maneno makali kuwa anajipendekeza.
Habari za kiintelijensia zilidai kuwa kati ya wanawake wanne aliowaacha
Tyson, pamoja na kutengana mwaka 2006 bila talaka, Mona ndiye amekuwa
akipewa pole badala ya wanawake hao wengine akiwemo Beatrice, Angel na
Lucy.
Kuna madai mazito yanayorushwa kwamba ishu ya mirathi ya Tyson inazidi
kuzua tafrani kila mmoja akijiaminisha kuwa ndiye mrithi halali.Baada ya
kuona maneno yanakuwa mengi ndipo Mona akacharuka na kuandika kwa kile
anachokijua juu ya ishu hiyo.
Aliandika: “Let me clear the air. Ni hivi, pamoja na ujinga tulioufanya
mimi na George katika maisha yetu, kwa macho ya kibinadamu utasema
alikuwa na mke mwingine lakini kwa macho ya ki-Mungu, mimi ni mke halali
wa George Otieno Okumu aliyelala.
Anayesema mke wa Tyson alijifungia ndani mimi nikawa nachukua pole
zisizo zangu, dah! Kwanza wanawake walikuwa wawili ndani siyo mmoja na
wote walijifungia ndani. Kwa nini? Ni Wakristo na wanaijua dini.
Waombolezaji walikuwa wakinipa pole mimi. Ni kwa nini?
Jiulize kabla ya kuropoka halafu wewe ni mwanamke kuna siku yatakukuta.
Nilienda (msibani) kutimiza wajibu wangu kama mke, ningelia peke yangu
kwetu mngenisema sana, nimekaa msibani naambiwa nachukua pole za bure.
Acha nikukumbushe maandiko... Alichokiunganisha Mungu?....(binadamu
asikitenganishe). Kilichofungwa duniani?.....(kimefungwa na mbinguni)
Nikupende, nikutunze hadi kifo?.....(kitakapotutenganisha).
Sasa kifo kimetutenganisha. Siku ya mwisho unadhani George ataitwa na
nani? Pamoja na mambo yake yote acheni nimlilie, he was a good father
kwa Sonia wangu especial miaka 5 ya mwisho wa uhai wake.
Acheni nimlilie, he was my best friend 1998-2014. Nime-share naye
kitanda 2000-2006. Nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu?
Ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa, usimcheke jua kuna sababu...na ni fundisho kwa wachukua waume za watu wote mjini.
Mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe na akifa? And for your info...msianze anajifanya mke sasa hivi ili apewe mali...
Sonia ni mali kubwa sana aliyoniachia, am so happy. Waache wao
wanaolilia kupewa pole wapiganie. Mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha,
sembuse tuliobaki?
“Niacheni nimlilie, waacheni fans wangu walie na mimi.”
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake walimshauri kuwa angenyamaza na
kuacha watu wazungumze kwani ni upepo tu unapita hivyo naye
aliwasikiliza na kuamua kuondoa maneno hayo katika kurasa zake kwenye
mitandao ya kijamii.
Tyson ambaye alikuwa bonge la mwongozaji wa vipindi vya runungani na
sinema za Kibongo alifariki dunia kufuatia ajali mbaya ya gari aina ya
Toyota Noah, iliyotokea eneo la Gairo mkoani Morogoro ambapo Jumamosi
iliyopita alizikwa kijijini kwao huko Kisumu nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment