
Tukio hilo limetokea usiku wa saa nane katika Kituo cha Polisi
Kimanzichana ambapo askari walikuwa lindo. Wakaja watu kama wanne hivi
kwanza wakiwa na mwenzao ana bandeji akijifanya majeruhi wamekuja
kuchukua PF3 wakamtibie. Kumbe ni majambazi wana mapanga wameyaficha
kwenye makoti.
Ghafla wakaanza kuyatoa na kuwashambulia askari na mgambo waliokuwa
kituoni. Askari Ngonyani ambae sasa ni marehemu alijitahidi kupambana
nao lakini alizidiwa nguvu na kumkata kata kwa mapanga pamoja na mgambo
wawili waliokuwa kituoni hapo.
Baada ya tukio hilo, majambazii hayo yalipora bunduki mbili za poliso
aina ya SMG na Magobore mawili yaliyokuwa yakihifadhiwa kituoni hapo.
Nje kulikuwa na sakari mmoja wakike alikuwa nje kwenye gari alijificha
kwa kuwa hakuwa na silaha muda huo, na ndiye aliyetoa taarifa kituo
kikuu cha Mkuranga mjini kwa OCD.
Bw. Ngonyani alifia hospitali ya wilaya akipatiwa matibabu, na mgambo
wawili wanaendelea na matibabu, ila mmoja hali yake imekuwa mbaya na
amehamishiwa Muhimbili.
No comments:
Post a Comment