KATIKA
MAISHA YA KIMAPENZI HAKUNA KITU KINACHOUMA KAMA KUSALITIWA, TENA
KUSALITIWA KUNAKOUMA ZAIDI NI PALE UNAPOBAINI MPENZI WAKO KAMPA PENZI
MTU UNAYEMJUA HALAFU UKIJILINGANISHA WEWE NA HUYO ALIYEPEWA UNASHINDWA
KUELEWA KILICHOMSHAWISHI MPENZI WAKO KUMPA PENZI HUYO MTU
Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa
wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo
mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake
Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio
kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimethibitisha hilo. Kama hali
yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako
kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama
ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.
Yafuatayo baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyafanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.
Kubaliana na kilichotokea
Kama keshakusaliti ni tukio ambao
limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika
lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.
Usijilaumu
Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta
kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu
akisema “najuta kumkubalia awe mpenzi wangu”. Kujilaumu kwa namna hiyo
hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.
Jitoe
Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo
wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao
ungempa basi uchukue kisha uufanyie kazi.
Pima ulivyoathirika
Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti
kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya
kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?
Mweleze ukweli
Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima
umweleze ukweli juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama
utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe
changamoto kwake.
Chunguza kwa nini kakusaliti
Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa
kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni
tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya
kimapenzi.
Usikubali akulainishe
Huenda huyo mpenzi wako ni msanii na
anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia
tukio hilo kiurahisi. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.
Amua kusuka au kunyoa
Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na
moyo wako. Uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila
shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi
nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye kwa kumkosa lakini kama unaona
moyo wako unamkataa, muache.
Msamehe
Kwa uamuzi wowote utakaochukua ni lazima
uwe tayari kumsamehe ili kuliondoa dukuduku lako rohoni. Kutokumsamehe
kunaweza kukufanya ukawa unaumia kila wakati na kukosa amani.
Iwe fundisho kwako
Chukulia tukio hilo kama fundisho kwako.
Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili
yasije yakakukuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa
kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa
kuchagua mwingine wa kuwa naye.
|
Saturday, 14 June 2014
JE WAJUA MAMBO YA KUFANYA BAADA YA KUSALITIWA NA UMPENDAE
About Jogoo Mtundu
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment