FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday, 19 June 2014

Cameroon imetupwa nje ya kombe la Dunia


Cameroon imetupwa nje ya kombe la dunia.
Cameroon imeondolewa katika kombe la dunia huko Brazil.
Hii ni baada ya kushindwa kwa mabao manne kwa moja na timu ya Croatia katika uga wa Manaus.
Cameroon walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji kumi baada ya mchezaji wa Barcelona Alex Song kuondolewa kwa kupewa kadi nyekundu.
Cameroon hawakuwapa Croatia upinzani mgumu katika mchuano huu wa kundi A.
Croatia sasa wana matumaini ya kuwania nafasi ya pili katika kundi hilo dhidi ya Brazil na Mexico ili kuendelea katika raundi ya pili.
Croatia wanajua kuwa mshindi katika mechi yao na El Tri, kama wanavyojulikana Mexico, ataendelea kwa michuano ya raundi ya pili ilhali Cameroon watamaliza kampeni yao dhidi ya wenyeji, Brazil.
Kikosi cha Niko Kovac kilishamiri katika mechi yao na Brazil katika mchuano wa ufunguzi hata ingawa walishindwa na hili lilionyeshwa hii leo pia walipoilemea timu ya Cameroon.
Katika dakika ya kumi na moja , Ivica Olic, mwenye umri wa miaka 34, akawa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika kikosi cha Croatia kuipatia timu yake bao kwenye kombe la dunia.

Mashabiki wa Cameroon
Ivan Perisic alimpa Olic pasi nzuri naye akamalizia kwa kufunga bao kwa mguu wake wa kushoto.
Perisic alizidi kuwa mwiba katika ngome ya Cameroon na akafunga bao lingine dakika tisa kabla ya muda wa mapumziko kwa kichwa.
Cameroon hawakuwa wametishia ngome ya Croatia kwa namna yoyote hadi wakati huo.
Mori na hasira zilizidi kuwapanda wachezaji wa kikosi cha Cameroon na hili likaletea Alex Song kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumgonga kwa kumbo mchezaji Mario Mandzukic hata ingawa Mandzukic hakuwa na mpira wakati huo.
Dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza, Croatia ilipata bao lake la tatu.
Bao hili lilisababishwa na kosa la kipa wa Cameroon, Charles Itandje, alipojaribu kuuondoa mpira nao ukamfikia Perisic.
Perisic, mwenye kasi, kutoka timu ya Wolfsburg ,Ujerumani aliipita safu ya Cameroon na kumpiga chenga Itandje na kisha akafunga bao .
Croatia ilizidi kuimiliki mechi hiyo huku Mandzukic akipata nafasi kadha za kuongeza mabao mengine.

Etoo hakucheza mechi hiyo
Mshambulizi huyo wa Bayern Munich, alifunga mabao mawili katika mechi hiyo. Bao lake la kwanza alilifunga kwa kichwa nalo la pili likatokana na kosa lingine lake Itandje.
Kipa huyo wa Cameroon aliutema mpira hafifu kutoka kwa mchezaji wa Croatia, Eduardo.
Mpira huo ukaanguka miguuni mwa Mandzukic ambaye hakusita kumwadhibu Itandje kwa kufunga bao lingine.
Matokeo haya yamedhihirisha umaarufu na ukakamavu wa timu ya Croatia na wanatarajia kuendelea kufunga mabao dhidi ya wapinzani wao Mexico ambao waliwalemea waandalizi wa kombe la dunia,Brazil.02:33 Cameroon bila
shaka sasa wanakuwa timu ya tatu kuelekea nyumbani na ya kwanza kutoka Afrika kufunganya virago.
02:31 Croatia 4-0 Cameroon
02:31 Mandzukic anafunga bao la nne la Croatia
02:31 Croatia 4-0 Cameroon 73''
02:19 Croatia 3-0 Cameroon
02:18 Mandzukic anafunga bao la tatu la Croatia
02:18 GOOOOAL
02:17 Itandje anakunguwaa lakini mpira unatoka nje na inakuwa KONA kuelekea Cameroon
02:16 Croatia 2-0 Cameroon
02:15 Srna anaupiga nje
02:13 FREEKICK kuelekea upande wa Cameroon nje ya eneo
02:12 Kipa wa Cameroon Itandje atajilaumu kwa bao hilo la pili ambalo hakuwa makini
02:11 Cameroon bila shaka sasa wanakuwa timu ya tatu kuelekea nyumbani na ya kwanza kutoka Afrika
02:09 Mandzukic amesalia peke yake na kipa wa Cameroon lakini anaupiga mpira nje ,,,,
02:09 croatia wanashambulia tena
02:09 Croatia 2-0 Cameroon
02:08 Peresic anaiweka Croatia mbele kwa bao la pili
02:08 GOOOAL
02:07 Croatia wanafanya mashambulizi
02:04 Kipindi cha pili kimeanza Cameroon 0-1 Croatia
01:45 Matumaini ya Cameroon kufuzu kwa raundi ya pili sasa yamepata pigo kubwa na itawalazimu kujifunga kibwebwe angalau kusaawazisha katika dakika 45 zzilizosalia.
01:45 Alexandre Song ametimuliwa uwanjani baada ya kumkomoa Mandzukic mgongoni na sasa Cameroon wamesalia wachezaji 10 uwanjani .
01:45 Cameroon 0-1 Croatia
01:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika .
01:44 Shambulizi la Cameroon likiongozwa na Aboubakar linakomeshwa
01:41 Cameroon sasa wanalazimika kucheza salio la mechi hii wakiwa watu kumi uwanjani.

Cameroon 0-1 Croatia
01:40 Song anaonekana kumgonga Mandzukic kutoka nyuma na refarii mreno Pedro Proenca
01:39 Alexander Song anaoneshwa kadi Nyekundu
01:36 Fastbreak kuelekea upande wa Cameroon lakini Song anaumega mpira na kugeuza na kuwa shambulizi kuelekea lango la Croatia akisaidiana na Mbia
01:34 Mandzukic anaongoza mashambulizi ambayo kipa Itandje anautema nje na inakuwa ni Kona.
01:33 Mbia anakuwa mchoyo na mpira na anaupoteza katika eneo la lango la Croatia
01:26 Iwapo Cameroon wataendelea kupena mpira hivi huenda wakawa timu ya tatu kuyaaga mashindano haya ya kombe la Dunia
01:25 Cameroon 0-1 Croatia
01:23 Stephanie Mbia anapoteza umiliki lakini Matip anapeana Freekick
01:22 KONA kuelekea Croatia
01:20 Mbia anapoteza nafasi nzuri ya kusawazishia Cameroon anaupiga mpira nje .
01:19 Luka Modric anaangushwa nje ya eneo na Matip
01:18 Mandzukic anaongosha mashambulizi katika lango la Cameroon
01:14 Croatia wanatawala mechi hii katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza
01:12 Croatia 1-0 Cameroon
01:11 Croatia wanapata bao la kwanza kupitia kwa Olic
01:10 BAOOOOOOOO

Timu ya Cameroon
01:09 Mario Mandzukic anamchenga Chedou
01:05 Mbia anaonywa na refarii Pedro Proenca
01:04 Vincent Aboubakar (Cameroon) anaangushwa na Cameroon inapewa freekick

Mashabiki wa Croatia
01:02 Cameroon inapata Freekick ya kwanza inayopigwa na A. Song
01:00 Mechi imeanza katika uwanja wa Amazonia ulioko Manus

Timu ya Croatia
00:59Timu mbili za kwanza katika kila kundi ndizo zinazosonga mbele
00:58 Timu zote kwa hivyo zitajitahidi kushinda mechi hii angalu kuokoa ari yao ya kufuzu kwa mkondo wa pili.

Etoo hatocheza dhidi ya Croatia
00:57Cameroon itakuwa bila ya nyota wake Samuel Etoo ambaye anauguza jeraha la goti
00:56 Cameroon kwa upande wake ilipoteza 1-0 dhidi ya Mexico katika mechi yao ya kwanza .
00:56 Croatia ilizimwa 3-1 na Brazil katika mechi ya ufunguzi
00:56 Croatia inachuana na Cameroon kwa mara ya kwanza katika fainali za kombe la dunia .

No comments:

Adbox