FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Wednesday, 5 March 2014

Alichosema Schmeichel kuhusu kuondolewa kwa wachezaji wanamuangusha Moyes




SetWidth638-PeterSchmeichel1812655iGolikipa wa zamani wa Manchester United  Peter Schmeichel anaamini David Moyes ni mtu sahihi kabisa kuiongoza klabu hiyo ya Old Trafford.
Mabingwa watetezi wa EPL wamekuwa na msimu m’baya zaidi katika kipindi cha miaka 20, lakini Schmeichel anaamini kocha wa zamani wa Everton sio tatizo linalopelekea timu kufanya vibaya.
Golikipa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Denmark aliambia Sky Sports News kwamba Moyes ndio kocha sahihi, lakini akamwambia kocha huyo afanye mabadiliko makubwa katika kikosi cha mashetani wekundu msimu ujao.
“Nadhani David ni chaguo sahihi kabisa,’  Schmeichel alisema.
“Ameonyesha uwezo wake, ana nia ya dhati na hali ya kupambana, anaweza kukaa sehemu kwa muda mrefu – alionyesha hizi sifa alipokuwa Everton.
“United inahitaji kocha ambaye atakaa na timu kwa muda mrefu lakini msimu huu umekuwa mgumu kwake.
“Atajifunza mwenyewe vitu vingi ndani ya muda, kila mtu atajifunza namna ya kuwa bora na timu itakuwa imara zaidi.
“Nafikiri anahitaji kusajili wachezaji kadhaa wengine – sijui wangapi ila anahitaji wachezaji!
“Lakini vilevile naamini anahitaji kuwaondoa wachezaji wengine kwenye timu. Kuna wachezaji wengi ambao kiukweli wanamuangusha.
“Kuwa mchezaji wa Manchester United , inaamanisha kubeba majukumu, inabidi ujitoe na kuipigania timu, siku zote hata kama mambo yanaenda visivyo, inabidi uendelee kujaribu.
“Nadhani mwishoni mwa msimu ujao wapo wachezaji watakaondoka.” 

No comments:

Adbox