Matonya ambae alipaswa kufanya show hiyo katika ukumbi wa Resort mjini Ludewa jana alikwama kufanya hivyo na badala yake alilazimika kukimbia eneo la ukumbi na kwenda kujisalimisha kituo cha polisi kufuatia jazba za wapenzi wake ambao walitaka arudishe fedha za kiingilio ambazo walitoa kiasi cha Tsh 4000 kwa kila kichwa .
Msanii huyo ambae alifika nje ya ukumbi huo toka mida ya saa 2 usiku akiwa katika gari ndogo aina ya Taxi nyeusi pamoja na promota wake wakiendelea kuchangisha fedha za madafu kutoka kwa wakazi wa Ludewa kwa maana ya kuwatoza kingilio huku Matonya akiwa mbele ya gari hiyo kwenye usukani akiendelea kuvuta sigara na kula kinywaji huku promota wake akiendelea kuwachojoa pesa za kiingilio mashabiki waliokuwa wakitaka kuona show hiyo.
Kama haitoshi mida ya saa 6 usiku hali ya wasiwasi ilianza kujitokeza ukumbini humo baada ya mashabiki kutoka nje ya ukumbi wakitaka msanii huyo kupanda jukwaani kutokana na muda kuendelea kuyoyoma bila ya Matonya kuingia ukumbini .
Hali hiyo ilipelekea vurugu za hapa na pale kutokea kwa mashabiki hao na uongozi wa ukumbi huo na baada ya muda polisi kufanikiwa kuzima vurugu hizo na mashabiki kulazimika kuingia ndani ya ukumbi kwa kutulizwa na nyimbo za wasanii wengine kama bolingo ,taarabu na nyimbo za Diamond .
Ili kuwa ni majira ya saa 7 .15 usiku ndipo matonya alipojitokeza ndani ya ukumbi huku meneja wa ukumbi huo akiwasha taa na kuwataka mashabiki kujiandaa kupata burudani ila haikuwa hivyo kwani Matonya alipanda jukwaani bila ya kisemeo (mic) na kuongea kwa sauti ya juu kuwa Mic haipo anaomba ipigwe nyimbo yake ili acheze na wadau wake hali iliyopingwa na kuanza mzozo ukumbini hapo.
Kutokana na mzozo huo ambao ulipelekea mashabiki kumtaka Matonya kuimba chini ya ulinzi bila ya kuwekwa CD katika radio ndipo Matonya alipotafuta upenyo na kukimbia ndani ya Ukumbi huo kutokana na kushindwa kutimiza matakwa ya wadau wake waliotaka kuimba live bila CD .
Kitendo cha Matonya kutoka nje ya ukumbi kiliamsha haliya vurugu ukumbini huku mashabiki hao zaidi ya 20 wakitaka kurudishiwa [pesa zao kwa madai kuwa zinatosha kwenda kulipa vibarua wa kupalilia mahindi shamba .
Madai hayo yalimfanya Matonya kuingia katika Taxi yake na wapambe wake na kukimbilia kituo cha polisi huku mashabiki hao wakilifukuza gari hilo kwa kutaka kumwadabisha Matonya kwa utapeli .
Pona ya Matonya ilikuwa ni kukimbia eneo hilo huku polisi wakilazimika kufika eneo hilo kuwatawanya mashabiki hao ambao baadhi walitangulia katika nyumba ya kulala wageni ya Malaika ambayo alifikia ili kumfanyia vurugu bila mafanikio baada ya msanii huyo kulazimika kuukumbia mji wa Ludewa usiku kwa usiku na kurejea Njombe .
Hata hivyo mbali ya kuwatapeli mashabiki hao bado msanii huyo anadaiwa kumliza mwenye muziki ambae ni afisa wa serikali wilaya ya Ludewa baada ya kumtumia kianzio cha Tsh 60,000 kati ya 150,000 za kukodisha vyombo vya muziki na kisha fedha hiyo ambayo aliituma kwa njia ya M- Pesa kuirudisha tena kwake .
Afisa huyo wa serikali amedai kuwa tayari amekwenda polisi kutoa taarifa ili kumsaka msanii huyo popote alipo na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria .
Jeshi la polisi wilaya ya Ludewa limethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuwa bila ya polisi kufika mapema eneo hilo msanii huyo angefanyiwa kitu kibaya zaidi na kuwa hadi sasa wanamsaka Matonya ili kufikia makubaliano na wadau wanaodai kutapeliwa fedha zao za kiingilio
No comments:
Post a Comment