
Waandamanaji Kiev
Tofauti za sera kati ya Marekani
na Umoja wa Ulaya kuhusiana na mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine
zimebainika wazi baada ya kuibuka mazungumzo ya siri baina ya maafisa
wawili wakuu wa kidiplomasia Kiev.
Mazungumzo yanayotajwa kuwa yalinaswa kisiri
kati ya wanadiplomasia wawili wakuu wa Marekani wakizungumzia mstakabali
wa Ukraine baada ya tandabelua la kisiasa yameiwacha marekani
ikionekana Mshari.
Nuland na Rais Yanukovich
''Yats ndiye anayepaswa Kuingia serikalini na afanye mazungumzo na Klitschko mara nne kila juma''
Nuland anasikika akiitusi Umoja wa Ulaya na kusema kuwa Umoja wa Mataifa ndiyo unaopasawa kuwa na usemi kuhusiana na hali ilivyo Ukraine kwani Kulinga naye 'Umoja wa mataifa ndio unapaswa kusaidia makundi ya upinzani kushikamana ''

Taharuki Kiev
Msemaji wa ikulu ya White House Jay Carney, amesema kuwa taarifa hizo ziliwekwa kwenye mtandao wa Twitter na afisa wa Urusi.
Kashfa hii ya kidiplomasia inatukia baada mshauri mkuu wa Rais Putin kulaumiwa na Marekani kwa kujiingiza katika siasa Ukraine.
Sergei Glazyev ameilaumu Marekani kwa kutoa mamilioni ya dola kwa vyama vya upinzani mbali na kuwakabidhi silaha.
Mshauri huyo wa Putina anasema hatua ya Marekani kuingilia maswala ya ndani ya Ukraine kimsingi inaipa Urusi uhuru na haki ya kuingilia kati.
Rais Putin anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Ukraine Viktor Yanukovych wakati wa michezo ya olympiki ya msimu wa baridi huko in Sochi .
No comments:
Post a Comment