CRAZY GK "EASTCOAST IMERUDI SASA TUTATUMIA ELIMU ZETU KUFANYA MZIKI WENYE LADHA"
Rapper, Gwamaka Kaihula aka King Crazy GK amewataka wapenzi wa East Coast Team kukaa mkao wa burudani baada ya members wa zamani wa kundi hilo AY na Mwana FA kumpa shavu kwenye kadhaa zake kadhaa.Akizungumza na Bongo5 leo, King Crazy GK amesema huu ni wakati wao wa kufanya kazi kama zamani kwa kutoa burudani nzuri ya muziki uliokwenda shule.
“Kwanza tumeanza kuongeza nguvu kwenye East Coast Team yetu mpya,sasa tunataka kama wanaume wawili na msichana mmoja. Pia Eastcoast Team ya zamani tumerudi tena pamoja na kuanza kufanya kazi pamoja. Tumeshaingia studio na kunapika mambo kwahiyo hivi soon utawaona AY na FA na wengine ambao wlikuwa wanaunda Eastcoast Team ya zaman,” amesema GK.
“Tutatumia shule zetu kufanya muziki wenye ladha,” ameongeza. “Sasa hivi tunatakiwa kufanya kitu kipya katika performance,tunataka kufanya vitu ambavyo watu hawataamini kama ni sisi. Unajua tunatakiwa kuwa kwenye level nyingine,sasa tukiwa kwenye ileile ina maana hakuna sababu yakurudi pamoja tena. GK wa sasa anapiga kinanda,anapiga gitaa, kwahiyo hii ni level nyingine.”
Source:Bongo5.com
No comments:
Post a Comment