Unaambiwa wiki moja baada ya staa wa
muziki Kenya (Jaguar) kuonyesha gari lake jipya aina ya Jaguar ambalo
alionekana nalo alipokwenda kufanya show, zimetoka picha za nje ndani za
gari analotembelea rapper CMB Prezzo wa Kenya ambae mara kadhaa
waliingia kwenye headlines na Jaguar kwa malumbano mbalimbali ikiwemo
kutambiana muziki, mali na uwezo wa kifedha.
Gari la Jaguar lenye thamani ya shilingi
Milioni 16 za Kenya ambalo liko mwisho wa hii post, aliiingia nalo
kwenye uwanja pembeni kabisa ya jukwaa alipokwenda kufanya show ambapo
alishuka kwenye gari wakati time yake ya kupanda jukwaani ilipofika,
alikua kalipaki karibu kabisa na ngazi za kupandia jukwaani.
No comments:
Post a Comment