Rais Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”
Rais
Jakaya Kikwete akimpa mkono wa pongezi Msanii mkali katika miondoko ya
Bongo Fleva, Abdul Nassib, Diamond kwa hatua aliyofikia.
“Diamond alilitangaza taifa letu kupitia shoo hiyo na muziki wetu wa
Tanzania, hivyo hatupaswi kuwa mbali na wasanii wetu kwani natambua
wazi Diamond bado yuko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za BET ambazo ni
tuzo kubwa sana nchini Marekani na naweza kusema kuwa hata kutambuliwa
kwake kuwepo kwenye tuzo hizo nalo ni jambo la kujivunia kwani uwepo
wake ni njia moja ya kulitangaza Taifa letu hata kama hatabahatika tena
kuchukua tuzo hizo,”
Diamond (kushoto) akiwa na mkali mwingine wa muziki kutoka Nigeria, maarufu kwa jina la Davido (aliye mbele pichani).
“Najaribu kuwatia sana moyo na kumwambia Diamond kuwa awe na
uvumilivu kwani nimeshaanza kuonyesha njia ya kumsaidia maana juzijuzi
nilimkuta Marekani na nilimkutanisha na mdau mkubwa sana wa muziki
duniani ambaye ndiye alimtoa Jay z, Usher Raymond na wasanii wengine
wakubwa na nilimuomba amsaidie kumwelekeza namna anavyoweza kukua kwenye
ulimwengu wa muziki”,“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa yetu,” alisema Rais Kikwete.
Diamond alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku chache baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi wa Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani hatapata chochote.
No comments:
Post a Comment