Jackline Wolper ni mmoja kati ya warembo wenye umaarufu mkubwa nchini na katika soko la Filamu za Tanzania.
Anamvuto unaokubalika na wengi na ameweza kujipatia umaarufu
mkubwa sana kupitia filamu alizoshirikishwa na alizozifanya chini
ya kampuni yake mwenyewe. Pia ni mwandishi mzuri wa Script na
muongozaji mzuri wa filamu....
Alizaliwa Moshi mkoani Kilimanjaro na kupata elimu yake ya
msingi katika shule ya msingi Mawenzi huko huko Moshi.Baadae
alipata elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Magreth
Ekenywa iliyopo jijini Arusha na inasemekana aliendelea na
masomo nchini Kenya.....
Rekodi zinaonyesha kuwa alitua jijini Dar kati ya mwaka 2005
na 2007 akiwa na jukumu moja tu la kusaka pesa.Kama ilivyo
ada kwa jamii ya watu wa kabila lake baada ya kufika jijini
Dar hakulaza damu, fasta alicheki michongo ilipo na kuanza
kuifanyia kazi..
Kujulikana kwake kulianzia pale alipoanza kupita mitaani
akitembeza bidhaa za mikononi na kuziuza kwa bei ya promosheni.
Hakuna aliyejua machina Wolper angekuja kuwa bonge la staa
nchini Tanzania...
Ni kipindi hiki ambacho wanaume walimchukulia poa na kumpita
bila hata salamu kama vile wafanyavyo kwa kina dada wanaotembeza
bidhaa za mikononi.Ni wanaume wachache sana ndo waliweza
kugundua uzuri wa Wolper na kumtupia maneno mawili matatu yenye
ushawishi wa ngono....
Baadae aliingia kwenye biashara za Saluni maeneo ya Tandale
jijini Dar kabla ya kujiingiza kwenye sanaa ya uigizaji....
Kipindi flani Wolper akiishi maeneo ya Mwenge alikutana na mtu
mmoja wa kabila lake aliyefahamika kwa jina la Injia Macha
ambapo jamaa huyo alianzisha utani wa kumuita mjomba lakini
baadaye ujomba ukapitiliza na akaanza kuomba kulila tunda....
Inasemekana kwamba jamaa alifanikiwa kulila tunda kwa kipindi
kirefu na aliponogewa alimuhamisha Wolper toka Mwenge alikokuwa
akiishi na dada yake na kumpangishia chumba cha kwanza maeneo
ya Sinza Mori....
Injinia huyo alimpatia Wolper gari chakavu aina ya Toyota
Celica ambapo baada ya siku kadhaa Wolper aliipiga bei gari
hiyo.....
Akiwa mitaa ya Sinza ndipo akakutana na mwanadada Lucy Komba
ambaye ni msanii wa filamu aliyemshawishi kujiingiza katika
tasnia hiyo....Kipindi hicho ilikuwa ni mwaka 2009.
Baada ya kupata mtonyo wa Movie, Wolper aliuchangamkia na kwa
mara ya kwanza akaonekana katika filamu ya 'Ama Zangu Ama Zao'
iliyofanywa na mwanadada Lucy Komba...
Baada ya hapo alianza kupata mialiko toka kwa watu mbalimbali
ili aweze kuigiza kwenye filamu zao.Alifanikiwa kukutana na
Director mkongwe,William Mtitu na marehemu Steven Kanumba na
kufanya filamu mbalimbali zilizomjengea jina katika tasnia
hiyo....
Baada ya kuanza kupata mafanikio, Wolper alizinguana na Injia
Macha ambaye alikuwa amempatia gari nyingine aina ya Toyota GX
100....
Mgogoro mkubwa uliibuka kiasi cha Injia Macha kuwatumia polisi
kumnyanga'anya gari hilo Wolper.Polisi walimkuta akiwa na gari
hilo maeneo ya Ilala ambapo alielezwa kuwa gari hilo
linatafutwa na mwenyewe na lina kesi katika kituo cha polisi
Oysterbay.
Wolper akiwa hajui kama mchongo huo ume injiniwa na Injia Macha
alitaka kuwavimbishia kifua maafande akidai kuwa gari hilo
alinunuliwa na mjomba wake na kadi anazo.Lakini alijikuta
akigonga mwamba kuondoka na gari hilo pale polisi walipomtaka
waende kituoni kulihifadhi gari hilo kisha akamlete huyo mjomba
wake pamoja na kadi za manunuzi ya gari hilo...
Wapekenyuzi wanaeleza kuwa kipindi hicho tayari Wolper alikuwa
na bwana mwingine na Injia Macha alishaushtukia mchongo na ndio
sababu alimfanyia umafia bila Wolper kujua....
Wolper akaingia mkenge, akamshtua bwana'ke mpya kuhusu polisi
wanachotaka kukifanya.Bwana'ke akamwambia asijali, wakutane
Oysterbay Polisi ili akalichukue hilo gari mbele ya maafande....
Kilichotokea ni kwamba baada ya Wolper kufikia kituo cha Polisi
alivutwa sikio na afande mmoja kwamba Injinia Macha yupo
kituoni hapo na anawasubiri kwa hamu yeye na bwanake waje na
documents za umiliki wa gari hilo hali iliyomfanya Wolper
aingie mtini....
Inasemekana kuwa kama bwana mpya wa Wolper angetokea kituoni
hapo angetiwa ndani yeye na Wolper kwa kesi ya wizi wa gari
lakini machale yakawacheza wakalala mbele.....
Baadaye Wolper alisikika kupitia Radio Clouds FM akitangaza kuwa
amedhulumiwa gari na mjomba wake ambaye alimuongezea pesa
kidogo katika manunuzi ya gari hilo lakini baadaye akawa
anamtaka kimapenzi na kumzushia kwamba amemuibia gari. Huu ndo
ukawa mwisho wa Wolper na Injia Macha.
Baada ya kutemana na Injia Macha, Wolper alipitia kwenye mikono
mingi ya kimahusiano lakini uhusiano mwingine uliompandisha
chati ni ule wa Abdallah Mtoro almaarufu Dallas....
Dallas akiwa hana jina la kutosha ndani ya jiji la Dar es
Slaam, ghafla alikuwa maarufu baada ya kutangaza ndoa na Wolper
na hasa pale alipompatia kiasi cha Dolla elfu 10 ( Tsh 16
Milioni) akampatie marehemu Sajuki kwa ajili ya matibabu. Kitendo
hicho kilimfanya Wolper awafunike mastaa wote wa kike akiwemo
Wema Sepetu......
Hata hivyo mahusiano ya Dallas kwa Wolper yalijaa utapeli
mwingi kwani wakiwa bado hawajafahamiana na Dallas ambaye
inasemekana ni mfanyabiashara wa 'Sembe' alimuingia kimafia
Wolper na kufanikiwa kumteka kimapenzi hadi akafunga naye
ndoa.....
Umafia alioufanya Dallas ni pamoja na kumpenyezea vitu vya
thamani kama vile magari ya kifahari na pesa za matumizi.
Kwa kuwa Wolper tangu anatoka Machame alijua anakuja mjini
kutafuta pesa, hakupoteza muda kutaka kujua mambo mengi kuhusu
Dallas. Alichoaangalia ni Dallas amekuja na mkono gani? Mkono
mtupu, mkono wa birika au mkono wa madini?
Alipogundua kwamba jamaa alikuwa na madini ya kutosha akajitoa
mzima mzima na kumkabidhi Dallas moyo wake wote , mwisho wa
siku akajikuta akiumbuka na kuambulia maumivu baada ya kumtambua
Dalls ni mtu wa namna gani.
No comments:
Post a Comment