Hehehe… heeeeee, heiiiya, acha nicheke miye mwana wa marehemu,
sijui wazazi wangu huko waliko wako katika hali gani, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu
awape kivuli chake siku ya kiama.
Waweza kuona nacheka ukadhani labda nimejawa na furaha, kumbe nafsi yangu
imejaa karaha, imekereheka kama siyo kukereheshwaKuna watu wengine kwa kweli kila kitu watende wao wakitenda wenzao huwa mwao,
hutaka kuicheza ngoma hata kama siyo ya kwao, upo?
Hivi inaingia akilini mama mtu mzima kutaka kuingilia ndoa ya mwanaye?
Tuchukulie mfano ni wewe mama ungekuwa na mtoto wa kike, ndoa yake ikawa inaingiliwa na mzazi mwenzako ungefurahi?
Nalisema hili kwenu nyie wenye tabia hii kwa kuwa huu ndiyo mwarobaini
wenye ladha chungu, lakini ndani yake unapata dawa ya kutibu maradhi
yako ya nyongo.
Kwa nini leo nimeamua kuyasema haya? Jamani kuna shoga yangu mmoja
kanijia mikono kichwani
machozi churuchuru nikadhani labda amefiwa, alichonieleza nilibaki
mdomo wazi kama siyo kupigwa na bumbuwazi.
Eti, mwanaye amekuwa akiendeshwa na mkewe kama gari bovu. Yaani mkwewe
amekuwa ndiye kinara wa nyumba na mtoto wake hafurukuti wala hatikisiki.
Kila siku mama anamwambia mwanaye ubaya wa mkewe lakini mtoto wala
hajali,
maneno yanaingia sikio hili yanatokea lile, hasikii kitu juu ya mkewe. |
No comments:
Post a Comment