
Serikali ya Rwanda
imedaiwa kuwazuia kupita nchini humo baadhi ya askari wa
jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliotoka kukisambaratisha
kikundi cha waasi wa M23 kilichokuwa Jamhuri ya Kimokrasia ya
Kongo (DRC) .....
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichozungumza jana na
MTANZANIA Jumatatu kimedai wanajeshi hao walitakiwa kuanza safari leo kuja nchini kupitia Rwanda lakini walizuiliwa bila sababu za msingi.
Chanzo hicho kilisema: "Hali ya usalama kati ya Tanzania
na Rwanda sio nzuri hata kidogo,Wanajeshi waliomaliza majukumu
yao nchini Kongo walikuwa waanze safari yao kurudi Tanzania
kesho ( leo ) kwa kupitia Rwanda, lakini katika hali isiyo ya
kawaida Rwanda wamekataa kupitisha askari hao nchini mwao.
"Mungu jalia viongozi wetu hekima na busara katika kuamua suala
hili zito kwa kuwa kama tutaingia katika vita wanaoteseka ni
watoto, wanawake na wazee ambao hawana uwezo wa kwenda kuishi
nje ya nchi, sala na dua zinahitajika sana kwa kuwa Mungu ndo kila kitu," mwisho wa kunukuu
Akizungumzia suala hilo, msemaji wa JWTZ,Luteni Kanali Erick
Komba alisema hafahamu kama wanajeshi hao walikuwa wameanza
kurejea nyumbani, hivyo apewe muda hadi atakapofika ofisini leo
ndipo atahakiki taarifa hizo.....
Mgogoro wa Tanzania na Rwanda ulianza kufukuta baada ya Rais
Kikwete kumshauri Rais Kagame wa Rwanda azungumze na waasi wa
serikali hiyo wanaofahamika kama FDLR, ambapo Kagame aligoma na
kuanza kumtolea maneno ya kashifa Rais Kikwete.....
Hata hivyo, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya M23 kusambaratishwa
na JWTZ walioungana na wanajeshi wengine wa vikosi vya Umoja
wa Mataifa (MUNUSCO).
M23 ni kikundi kilichodaiwa kuundwa na askari wa makabila ya Rwanda, jambo linalopingwa vikali na Rais Kagame.....
Katika hatua nyingine, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
mataifa, Benard Membe alikiri kuwapo kwa uhusiano mbaya kati ya
Tanzania na Rwanda.Kauli hiyo aliitoa bungeni mjini Dodoma
hivi karibuni alipowasilisha bajeti ya makadirio ya mapato na
matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2014/ 2015.
Alisema uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa mbaya kwa sababu kuu mbili kubwa.
"Ni kweli tuna uhusiano mbaya na Rwanda, kwanza tunaogopana kwa
kuwa kila upande mmoja ukiongea na hasimu wa mwenzake
inaonekana kama kuna hujuma inataka kufanywa.
"Pili kuna watu wanapeleka maneno ya chokochoko.Pia M23 ni
wanamgambo wa Rwanda na kuna ushahidi kwamba Rwanda ilipeleka
wanajeshi kuwasaidia wakati wa mapigano na serikali ya DRC
yakiendelea, ushahidi huo upo," alisema Membe
Tanzania ina historia iliyotukuka katika ukombozi wa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na ndio maana ilichaguliwa kuongoza majeshi ya kulinda amani DRC
Mwaka 2008, makamanda na wapiganaji wa JWTZ waliongoza vikosi
vya washirika katika kazi ngumu ya kumng'oa kanali Bacar wa
Visiwa vya Comoro na Anjouan.
Uamuzi wa AU kuipa kazi hiyo Tanzania kuongoza mapambano hayo haukuwa wa bahati mbaya, bali ulitokana na kutambua kuwa ni nchi iliyoshiriki na kufanikiwa katika vita mbalimbali ya ukombozi


No comments:
Post a Comment