Mwanamke wa Nigeria aliyejitambulisha kwa jina la Mercy James amesimulia
tukio la ajabu la kujifungua salama mtoto wa kike baada ya kuwa
mjamzito kwa kipindi cha miaka 14. Mtoto aliyeamua kumuita ‘Miracle’
Kwa mujibu wa Vanguard, Mercy alieleza kuwa alianza kujisikia dalili za
ujauzito miaka 14 iliyopita lakini awali dalili hizo zilikuwa
zinabadilika na mara nyingine anaingia katika hedhi kwa siku moja,
lakini hali ilianza kuwa serious miaka miwili baadae alipoenda hospitali
na kuhakikishiwa kwa vipimo kuwa ni mjamzito.
“Nilienda tena kwa tabibu miaka miwili baadae na kumlalamikia kuhusu
maumivu niliyokuwa nayapata, aliniambia tena kuwa sina tatizo la tumbo
na kwamba huo ulikuwa ujauzito. Alinishauri niendelee na maombi ili
Mungu aniepushe na mikono ya shetani.” Mercy alisimulia.
Anaeleza kuwa alikuwa anatumia madawa mengi ya kutibu magonjwa ya tumbo lakini hali yake haikubadilika.
Hali iliendelea hivyo hadi ilipofika June 7 mwaka huu ambapo alienda
tena katika hospitali hiyo akiwa analalamika na kusikia kila dalili za
kitu kutaka kutoka mwilini mwake, lakini hakufahamu kuwa hiyo ingekuwa
siku ambayo angejifungua mwanae wa kike, ‘Miracle’.
“Kisha Mungu aliamua kunifuta machozi. Katika siku niliyojifungua
mwanangu wa kike, mwanzo nilihisi ni minyoo inataka kutoka kwenye mwili
wangu bila kufahamu kuwa yule alikuwa mtoto. Hivi ndivyo nilivyomwambia
mkunga. Lakini baada ya kunipima alianza kuniambia nisukume.
Nilimpotezea. Baadae nikaishiwa fahamu kama dakika 15 na nilipopata
fahamu, nilisikia mtoto Analia. Nilishangaa sana na kuchanganyikiwa
nilipomuona mwanangu. Sikuweza kuamini macho yangu.” Mercy aliendelea
kusimulia tukio hilo.
Naye tabibu wa hospitali ya kanisa la ‘Celestial Church Of Christ,
Parokia ya Kadoso ambapo Mercy alijifungulia, aliyetajwa kwa jina la
Ajegunle aliliambia Vanguard kuhusu hatua zote alizopitia hadi
kujifungua mwanae huyo na jinsi yeye binafsi kama mkunga alivyohusika.
Marafiki na ndugu wa mwanamke huyo walitoa ushuhuda pia kwa gazeti la Vanguard la Nigeria kuhusu tukio hilo la kushangaza.
No comments:
Post a Comment