Alisema eti aachwe kwanza, eti baada ya ule mkasa hataki kabisa kusikia habari za mapenzi.Amini usiamini , haukupita muda mrefu skendo za mapenzi zikaanza kuvuma tena.
Tukaanza
kusikia habari za kina fulani zikihusishwa na yeye.Alianza
yule jamaa handsome asiyekuwa na jina kubwa.Bila kujulikana
alipotokea akaibuka na kusema alikuwa na mahusiano na Lulu
Michael na alikuwa katika mchakato wa kumuoa. Baadaye Lulu
akamkana, yakaisha.
Likaja
swala la Diamond, sukari ya warembo.Yeye alisema aliwahi kushea
shuka moja na Lulu. Wote tuliamini. Kwani wewe humjui Diamond?
Huwa hafanyi kosa.
Diamond
wa Jack Wolper, Peniel Mungirwa, Irene Uwoya, Aunt Ezekiel na
Jokate Mwegelo. Kwa namna gani akisema kashea shuka na
msichana ukatae? Kwanza wasichana wenyewe hujisikia faraja na
fahari kuhusishwa naye.
Lulu
sasa ameibuka na stori ya jamaa mwingine aitwaye Nando
aliyekuwa mshiriki wa Big Brother mwaka jana. Bila kuuma maneno,
jamaa kasema Lulu ni demu wake. Baada ya Lulu kupigiwa simu
alisema aulizwe Nando, atakachosema yeye hana usemi.
Nando
akaendela kusisitza kuwa Lulu ni demu wake.Cha kushangaza
baada ya Nando kukubali, siku tatu baadae Lulu kamkana jamaa.
Eti kasema jamaa anatafuta kiki. Mwanzo alipoulizwa na kusema
aulizwe nando ndo mwenye jibu alimaanisha nini?
Eti
anasema ni kweli alitongozwa na Nando na akamkubali ila
hawakuwahi kuvuliana nguo. Sisi tutaamini vipi? Ya ndani hubaki
siri za wa ndani. Sisi wa nje tutajuaje kama hawakufanya
chochote.?
Kwanza
katika dunia ya leo, dunia iliyooza na kuvaa vimini, mwanamke
akitongozwa maana yake nini? Tena staa kama yeye? Mwenye lundo
la skendo za mapenzi? Akitongozwa na kukubali kinachofuata ni
nini?...Kwa hili Lulu nakuona haupo Serious.
Lakini
ni kwa nini Lulu anakuwa na majibu ya kutatanisha juu ya
mahusiano yake? Au ana mtu mwingine na alitaka Nando awe wa
akiba? Au alidhani akiwa na Nando kwa sababu jamaa siyo staa
itakuwa siri hivyo kufungua mianya ya michepuko?
Kwa
nini mwanzo Lulu alipohojiwa alionekana kama kuridhia kila
jibu litakalotolewa na Nando, ila baadaye akakana? Nani alihoji
kama wametembea naye hata ajishuku hivyo? ...Kwa hili Lulu nakuona haupo Serious.
No comments:
Post a Comment