Hebu fikiria, umetoka na mkeo kwa ajili ya mlo wa jioni. Mgahawa ni mzuri uko pembezoni mwa bahari. Upepo mwanana unazifurahisha nyoyo zenu. Mnakumbushana milima na mabonde mliyopitia. Mnacheka kwa furaha huku mkipongezana na kumshukuru Mungu kwa jinsi mnavyovumiliana na kupenda.
Mnaongelea kuhusu mipango yenu kazini, na namna ya kuboresha miradi yenu binafsi. Mkiwa katikati ya maongezi, anatokea jamaa mmoja. Ghafla anaanza kumrapua vibao mkeo eti anaringa sana.
Humfahamu wala hujawahi kumuona. Siku hiyo ndio unamuonba kwa mara ya kwanza na hii ndio picha yake hali baada ya kumaliza kumpiga mkeo
Je utamfanya nini ili kumzuia asiendelee kumuumiza mkeo?
No comments:
Post a Comment