Hili Bunge la Katiba kwa kweli limefichua Mengi sana hasa kwetu sisi ambao tumezaliwa miaka ya tisini..Nilikuwa sijui kuwa Tanzania kuna mfungwa wa kisiasa. Zipo taarifa kuwa Abdu Jumbe, aliyekuwa raisi wa Zanzibar ni mfungwa akizuiliwa huko Kigamboni na hatakiwi kutoka wala kutembelea Zanzibar kwa kosa la kudai mamlaka kamili ya Zanzibar.
Kama huu ni ukweli basi huu ni wakati muafaka kwa Wazanzibari wadai kwa namna wanavyoona wao wanafaa uhuru wa mtu wao, aliyekuwa raisi wao na sasa yupo kizuizini nje ya mipaka yao kwa kutetea maslahi ya waliomchagua.
No comments:
Post a Comment