FACEBOOK

LightBlog

Breaking

LightBlog

Thursday, 10 April 2014

LADY JAYDEE ASHIRIKI KWENYE WIMBO RASMI WA KOMBE LA DUNIA

Msanii mkongwe wa muziki nchini Judith Mbimbo maarufu kama Lady Jaydee ameshiriki kuimba wimbo maalum wa kombe la dunia 2014 akishirikiana na David Correy na rapper wa Kenya, Octopizzo

Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo ‘akichana’ kwa Kiswahili.

Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza wiki hii jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

No comments:

Adbox